Bukobawadau

KAMPENI ZA URAIS ZA DK MAGUFULI NI MWENDO MDUNDO MTWARA

 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Mashujaa mjini Mtwara leo, ambapo alijinadi na kuwanadi wagombea ubunge pamoja na wagombea udiwani katika Manispaa ya Mtwara.

Dk Magufuli tayari hadi sasa amefanya mikutano ya kampeni katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Mtwara. ambapo aakishinda uchaguzi ameahidi mambo mbalimbali kama vile ile ya bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne, kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay mkoani Ruvuma, kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na kutoa sh. mil. 50 kwa kila kijiji za kuwakopesha wanawake na vijana kuendeleza miradi na biashara zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na ahadi mbalimbali zilizotolewa na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara leo
 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Mashujaa mjini Mtwara leo, ambapo alijinadi na kuwanadi wagombea ubunge pamoja na wagombea udiwani katika Manispaa ya Mtwara.
 Dk Magufuli akimsaidia hela mtoto Riziki Faraji za kununulia sare ya shule alipomuona wakati msafara wake ulipozuiwa na wananchi katika Kijiji cha Kitama A, mkoani Mtwara
 Wazee wakisikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akijinadi katika Kijiji cha Chiungutwa  wilayani Masasi, Mtwra leo
 Dk Magufuli akishangiliwa na wananchi katika Kijiji cha Nangaga wilayani Newara, Mtwara
 Dk Magufuli akifurahi baada ya wazee wa kimila  kumkabidhi siraha za jadi wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja mpira wa Newara mjini

 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Newara Mjini, George Mkuchika wakati wa mkutano huo.
 Mgombea ubunge Jimbo la Newara Vijijini Rashid Akber akiwa na furaha alipokuwa akinadiwa na Dk Magufuli mjni Newara

 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Kijiji cha Kitama A, wilayani Newara
 Wananchi wakishangilia baada ya kumona Dk Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa kampeni mjini Tandahimba
 Katika mkutano wa Tandahimba
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Tandahimba, Shaibu Likumbo
 Ni furaha iliyoje kwa wananchi walipomuona Dk Magufuli mjini Tandahimba

 Dk Magufuli akihutubia katika Jimbo la Nanyamba, wilayani Tandahimba
 Picha za Dk Magufuli zikiwa zimeupamba mkutano wa kampeni katika Kata ya Ziwani Mtwara Vijijini leo

 Dk Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Ziwani, Mtwara Vijijini.
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Ziwani Mtwara Vijijini
 Jamaa mwenye asili ya kimasai akicheza kwa furaha baada ya kumuona Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwra.
 Dk Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mashijaa mjini Mtwra
 Dk Magufuli akicheza pamoja na wananmuziki wa bendi ya Yamoto iliyokuwa ikitumbuiza kwenye mkutano huo. Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba akitumbuiza katika mkutano wa kampeni wa CCM mjini Mtwra
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya wenye ulemavu nchini, Amon Mpanju akielezea jinsi Serikali ya CCM inavyowajali watu wenye ulemavu hivyo kuwataka wananchi kumchagua Dk Magufuli katika uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
 Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini,Husnein Murji akimtuza Amon Mpanju

 Dk.Magufuli akimnadi Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Murji
 Dk Magufuli akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiondoka baada ya kumaliza mkutano kwenye Uwanja wa Mashujaa

Next Post Previous Post
Bukobawadau