Bukobawadau

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE NDANI YA CHIMALA,MBARALI,MAKAMBAKO NA MAFINGA,KESHO KUUNGURUMA IRINGA MJINI

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaiambisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Mafinga mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
 Mmoj wa Waangalizi wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,akifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Makambako jioni ya leo Septemba 27 mkoani Iringa
????????????????????????????????????
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up mbele ya wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  ambaye anashuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vyaWambi  mjini Mafinga mkoani Iringa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.

Dk. John Pombe Magufuli amewaambia wakazi hao wasihadaike na maneno ya kisiasa yanayotolewa na vyama vingine kuwa nchi ya Tanzania haijapiga hatua ikiwa chini ya utawala wa CCM wakati maendeleo yanaonekana wazi na nchi inazidi kusonga mbele kwa mambo mengi ikiwemo amani na utulivu wa nchi.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa  Chimala,Mbarali mkoani Mbeya alipokuwa akielekea mkoani Iringa kuendelea na kampeni zake.
 gombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akionesha hisia zake mara baada ya kuonana uso kwa uso na Kada Mkongwe wa chama cha CCM Ndugu Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kada Mkongwe wa chama cha CCM Ndugu Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni,huku Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Ndugu  Bulembo akifuatilia kwa makini
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini katika viwanja vya Barafu mjini Rujewa,wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga a.k.a Jah People akimuombea kura  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini Ilembula leo Septemba 27 mkoni Mbeya
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Injinia Gerson Rwenge,katika mji wa Ilembula
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mjini Makambako kwenye uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 wakazi wa Makambako wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipanda jukwaani kwa kuruka ruka kuonesha yuko fiti kuwatumikia wananchi kwa namna yoyote ile.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah Bulembo akiwahutubia wakazi wa Makambako kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli leo Septemba 27 mkoani Iringa
 Dkt Magufuli akiwasalimia wananchi wa Makambako kabla ya kuanza kuwahutubia na kuwaomba kura
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Makambako gombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaimbisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wananchi wa mji wa Makambako wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuwaomba wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 27 kwa kumpiga kura ya ndio na hatimae aibuke mshindi kwa nafasi ya Urais

Next Post Previous Post
Bukobawadau