Bukobawadau

MAGUFULI ASOMEKA VYEMA NKENGE-BUNAZI

Umati wa wananchi Wilayani Missenyi wakimpungia Mikono Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo lake la Nkenge ,Uliofanyika Bunazi katika Uwanja wa halmashauri mapema ya leo Jumanne Sep 22,majira ya saa mbili na nusu asubuhi.
 Wananchi wakiendelea kumsikiliza Mh. Magufuli wakati akiwahutubia katika mkutano wake wa Kampani mapema ya leo.
Akiwahutubia wananchi wa Missenyi Dkt Magufuli amesema atashughulia swala la mogogoro ya Ardhi, maswala ya uhamiaji pamoja na kushuka kwa bei ya zao la kahawa
 Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano huo
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya fupi ya Mgombea Ubunge jimbo la Nkenge Dr. Diodorus Buberwa Kamala.
Mwanadada akimsikiliza kwa makini Dk John Magufuli
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo akiwahutubia mamia ya wanachi waliohudhuria Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Mh.Magufuli ,Wilayani Missenyi
 Sheikh wa Wilaya ya Missenyi,Sheikh Abdul Chagulani akimuombea Dua Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiteta jambo na Sheikh wa Wilaya ya Missenyi,Sheikh Abdul Chagulani
 Sehemu ya wadau waliofika katika mkutano huo leo
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Nkenge aliyekuwa Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala.
  Pichani ni sehemu ya Wagombea Udiwani walioshiriki katika mkutano wa kampeni za CCM Wilayani Missenyi uliofanyika Bunazi mapema ya leo
 Sehemu ya Wagombea Udiwani kupitia CCM jimbo la Nkenge.
Mkutano ukiendelea na Ulinzi ukiwa umeimarishwa eneo la tukio
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Mama Constancia Buhiye
 Taswira mara baada ya Mkutano huo kumalizika ambapo  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli ameendelea na Kampani zakekatika Wilaya za Karagwe na Ngara
 Wananchi wa mji wa Ngara na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya posta mjini humo,huku wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais na kuiongoza nchi Tanzania katika awamu ya tano.Dkt Magufuli amekamilisha mikutano yake ya kampeni zake katika mkoa wa Kagera wenye jumla ya majimbo 9 ya Uchaguzi. PICHA NA MICHUZI JR-KAGERA
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.Dkt Maguful kwa siku mbili mfululizo ameweza kukamilisha mikutano yake kwenye Wilaya  zote za Mkoa wa Kagera,ambapo kesho anaelekea mkoani Geita kwa ajili ya kujinadi kwa wananchi wa mkoa huo ili waweze kumpigia ya kuwa Rais wa awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwafafanulia kwa umakini mkubwa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema leo mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Sehemu ya umati wa watu ulikuwa umefika kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema leo mchana kwenye uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyera mkoani Kagera.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema leo mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Wakazi wa Ngara na vitongoji vyale waliokusanyika kwenye viwanja vya Posta mjini Ngara jioni ya leo wakishangilia jambo,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Wananchi wa Ngara wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kampeni
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Kayanga,Karagwe mjini asubuhi hii kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Mashujaa mjini Misenyi asubuhi hi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
 wakazi wa mji wa Misenyi  katika viwanja vya mashujaa wakishangilia huku wakiendelea kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,alipokuwa akijinadi kwa kumwaga sera zake na kuomba watanzania wamchague kwa ridhaa yao ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya Tano
Next Post Previous Post
Bukobawadau