Bukobawadau

MATUKIO YALIYOJIRI MJINI BUKOBA SIKU YA UTALII DUNIANI 2015

Mjini Bukoba Maadhimisho ya siku ya Utalii kwa mwaka 2015 yalifanyika siku ya Jumamosi  kwenye Viwanja vya fukwe za Kiroyera Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ambapo kila nchi mwanachama wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) husherekea siku hii, kwa lengo la kuweka uelewa kwa Jamii kuhusu umuhimu wa utalii na thamani yake, kijamii, kisiasa, kitamaduni na kiuchumi.,Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni "Mamilioni ya Watalii ni Mamilioni Fursa"
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Katibu Tawala Mkoa wa Kagera(RAS) Bw Nassoro Mnambira  pichani kushoto akikagua mabanda ya maonyesho wa wadau wa utalii.
 Mchoro wa Nyumba ya asili ya “majani full suit” maarufu kama “Mushonge museum”
 Muonekano wa bidhaa mbalimbali


 Mgeni rasmi Bwana Bw Nassoro Mnambira akikagua banda la wawezeshaji na wauzaji wa tiketi za usafiri wa ndege, Bukoba Machinery & General Supplies Ltd na Auric Air
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Katibu Tawala Mkoa wa Kagera(RAS) Bw Nassoro Mnambira akikagua banda la ELCT Hotel
 Banda la maonesho la Kampuni ya Utalii ya Kiroyera Tours
 Mkurugenzi wa Fiosmin Hotel Bi Lilian Rwakatare mdau wa Utalii na mratibu wa maadhimisho hayo akitolea jambo ufafanuzi
 Mkurugenzi wa Kiroyera tours Bi Mary Conso Kalikawe akielezea juu ya Umuhimu wa kuadhimisha siku ya utalii duniani ,historia ya siku hiyo Mji Mjini Bukoba na Umuhimu wa maadhimisho ya Utalii Mjini Bukoba
 Akiongea kuhusu historia ya maadhimisho hayo Mjini Bukoba ,mtayarishaji wa maadhimisho hayo Bi Mkurugenzi wa Kiroyera tours Bi Mary Conso Kalikawe amesema: 'Mji wa Bukoba ulianza kuadhimisha siku ya utalii duniani mwaka 2002 na kuendelea kufanya hivyo kila mwaka hadi mwaka 2008.
 Aidha Kulikuwa na chama cha kuendeleza utalii mkoa wa Kagera maarufu kama Kagera Tourism Development Association ( KATODEA) ambacho kilifanya mchango mkubwa na katika mwaka 2006, Mkoa wa Kagera ulipata fursa adimu ukawa mkoa ulioadhimisha siku ya Utalii Duniani kitaifa hapa mjini Bukoba. Huo ndio ulikuwa ufunguo wa kutambuliwa Mkoa wa Kagera katika ramani za utalii nchini Tanzania. KATODEA imekuwa haiendelei kwa muda mrefu sasa
 Kuhusu Umuhimu wa kusherekea Siku hii Mjini Bukoba:Kuanzia mwaka 2002 utalii ulikua na kuanza kuleta mabadiliko endelevu mwaka hadi mwaka. Mahoteli  kama Walkgard, Kolping, Victorious Pearch, Smart, Yaasila Top kwa sasa Bukoba Coop na nyingine nyingi zilijengwa. Kiroyera Tours, Walkgard hotel, Tausi Curio na Hoteli ya Kamachumu Inn walikuwa mstari wa mbele kutangaza utalii. ‘Tausi curio shop’ ilikua haraka na kuwa na maduka matatu yenye kazi za mikono ya hali ya juu na ya kuvutia watalii  katika mji wa Bukoba.  Watalii walianza kutembelea vivutio mbali mbali vilivyoko Manispaa ya Bukoba, Bukoba vijijini, wilaya ya Muleba na wilaya ya Misenyi. 
Kazi kubwa ilifanywa ya kuainisha vivutio mbali mbali vilivyomo Mkoani Kagera kwa msaada wa wizara ya mali asili na utalii. Vivutio pia viliendelezwa kwa kuwekewa barabara za kupitia watalii, kutengeneza ratiba za matembezi zinazounganisha vivutio hivyo na kuvitangaza katika maonesho mbali mbali kama saba saba hapa Bukoba na maonesho ya utalii kitaifa (huko Arusha na Dar es Salaam) pia maonesho ya kimataifa (Spain, Uingereza, Milani, Belgium, Ufaransa na Marekani). Vijitabu vya vuvutio hivi viliandikwa  pia na kusambazwa.  Katika vivutio hivi kuna mvuto wa Ziwa Victoria kwenda kisiwa cha Musira,  kisiwa cha hifadhi ya Rubondo (Rubondo Island National Park) na vinginevyo
Kuna msitu wa Kyamunene na  maporomoko ya maji na pango karibu na Bukoba na maporomoko yam to Bugonzi huko Kamachumu; Wahunzi wa vyuma wa Itahwa na utaalamu wa asili wa vyuma wa Maruku Zamadamu Katuruka; Mapango ya michoro ya kale ya Bwanjai –Mugana; chakula na mapishi ya asili, ngoma na nyimbo za kitamaduni Gera, maarufu kama” kwa mama Kisha”  na nyumba za asili za “majani full suit” maarufu kama “Mushonge museum” huko Kanoni   Kamachumu. Kwa juhudi hizi Kisiwa cha Rubondo ambacho hapo awali kilikuwa kinapata wageni kwa nadra sana, kwa sasa huwa kinafikia kukataa kupokea wageni ili kulinda kisizidi viwango na kuathiri uhifadhi wa wanyama na mazingira.
 Nyumba za asili za “majani full suit” maarufu kama “Mushonge museum” huko Kanoni   Kamachumu. Kwa juhudi hizi Kisiwa cha Rubondo ambacho hapo awali kilikuwa kinapata wageni kwa nadra sana, kwa sasa huwa kinafikia kukataa kupokea wageni ili kulinda kisizidi viwango na kuathiri uhifadhi wa wanyama na mazingira.
Muendelezo wa matukio ya picha kutoka viwanja vya Kiroyera Tours vilivyoko katika fukwe za ziwa Victoria, barabara ya Forodhani – Shore Road Kata Bakoba
 Hotuba fupi kutoka kwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Katibu Tawala Mkoa wa Kagera(RAS) Bw Nassoro Mnambira
 Burudani ya Ngoma
 Mkurugeni wa Kiroyera tours katika picha ya pamoja na Ma Anastazia na mwanae wa kijijini Gera mara baada ya kutunukiwa Chti maalum
 Mdau wa Utalii na Mjasiliamali kutoka kijijini Gera Ma Anastazia akipokea Cheti maalum  
Afisa wa Marine Services Bw. Mathew Mathias akipokea cheti maalum
Mzee Leonidas Muhanika na mkewe wa Kamachumu Mushonge Museum mara baada ya kukabidhiwa Cheti.
Siku ya Utalii Dunia  Mjini Bukoba limefanyika Kongamano ambalo limewashirikisha watu 15 ambao mawazo yao wameyaelekeza kwenye Utalii na Siku ya Utalii Duniani waweze kukutana kwenye ukumbi wa juu Kiroyera Tours na kubadilishana mawazo na mitazamo mbali mbali. Mazungumzo yataelekezwa kwenye dhana ya siku ya Utalii hususani utalii katika mkoa wa Kagera. Lengo ni kuondoka kwenye kongamano hili na maazimio kadhaa yatakayosaidia kuendelea kukua kwa kasi kubwa utalii mkoani Kagera.
 Muonekano wa jiwe la msingi lililo zinduliwa rasmi na Mgeni rasmi Bw Nassoro Mnambira
 Staff wa Victorious Pearch Hotel
  Mwakilishi wa ELCT Hotel Bukoba Aristides Musheshe (katikati) mara baada ya kukabidhiwa cheti
Katikati ni mwakilishi wa kisiwa cha hifadhi ya Rubondo (Rubondo Island National Park)
 Maelezo kutoka kwa msemaji wa ELCT Hotel
 Mgeni rasmi akikabidhiwa risala .
 Katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Kampuni ya Auric Air
 Ukuaji wa Utalii Mjini Bukoba:Ni vyema kusema Bukoba inapokea watalii halisi kutoka nje 2000 kwa mwaka, ambao wanafika Bukoba kwa ajili ya utalii tu. Kati ya hawa kuna wanaotaka kuona na kutembelea vivutio vilivyopo hapa Bukoba, na baadhi yao ni wapita njia, wengine wanatafuta usafiri, wengine wanatafuta huduma ya malazi na baadhi wanataka kuishi kwa muda katika jamii ya Bukoba na kufanya kazi za kujitolea. Ni mara nyingi sana kuona magari yakusafirisha watalii kutoka Uganda na Rwanda yakiwa Bukoba. 
 Ukweli ni kuwa nchi ya Uganda hupata watalii wengi kuliko nchi ya Tanzania. Baadhi ya watalii kutoka Uganda hupitia mjini Bukoba wakiwa wanaelekea kwenue mbuga za wanyama za Serengeti na Ngorongoro. Huduma ya usafiri ni muhimili kwa utalii. Wasafirishaji ni pamoja na kampuni ya ndege ya Auric, Precision Air, huduma za usafiri wa majini MV Victoria na sasa MV Serengeti ambayo kwa sasa ni chaguo la watalii wengi wa Bukoba. Pia kuna usafiri wa njia ya barabara Taxi pamoja na mabasi na boda boda.
 Maswala ya nyama choma yakiendelea fukweni Kiroyera
 Wanafunzi wa Chuo cha King Rumanyika katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi na Mkurugenzi wa Kiroyera Tours
 Taswira ndani ya banda la ELCT Hotel
 Mikufu iliyotengenezwa kiasili
 Muonekano wa washiriki wa maadhimisho ya siku ya Utalii Duniani, Mjini Bukoba
 Sehemu ya wanafunzi wa Chuo kinachotoa Diploma ya Elimu cha King Rumanyika kilichopo maeneo ya Nshambya mjini Bukoba
Burudani za hapa na pale zikiendelea
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo.
 Billion Tourists – 1 Billion Opportunities (Hii ndio kauli mbiu ya siku ya Utalii Duniani 2015) *Mabilioni ya watalii ni mabilioni ya Fursa
 Staff wa Kampuni ya Kiroyera Tours wakitoa huduma meza kuu.
 Baadhi ya wanahabari walioshiriki Maadhimisho hayo
Wauzaji wa bidhaa mbalimbali
 Picha ya awali Mkurugeni wa Kiroyera Tours akiwa na baadhi ya wanakamati wa maandalizi ya siku ya Utalii Duniani
 Kamati ya maandalizi ya Shughuli katika picha ya pamoja.
 Pichani anaonekana mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Auric Air
Credit kwake Bi Mary Conso Kalikawe pichani kushoto,Mkurugeni mwendeshaji Koroyera Tours

BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241

Next Post Previous Post
Bukobawadau