Bukobawadau

ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU TANO,MAGUFULI AENDELEA KUITIKISA KANDA YA ZIWA,AFANYA MIKUTANNO YA KAMPENI GEITA VIJIJINI,NYANG'WALE NA SENGEREMA

Mgombea Urais kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Sengerema jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo.Katika mkutano huo wa kampeni Dkt Magufuli amezishauri halmashauri nchini kuacha tabia ya kukopa pesa kutoka katika taasisis za kifedha na kulipia fidia za wananchi ambao serikali inataka kutumia maeneo yao kwa ajili ya huduma za kijamii. 

Akiomba kura katika wilaya mpya ya Nyang'wale mkoani Geita,Dkt Magufuli ametumia jukwaa hilo kukataza mpango wa kukopa pesa kutoka kwa taasisi za kifedha,ambapo wamekua wakitaka riba kubwa  ili kuweza kulipa fidia kwa wakazi ambao wameamishwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za halmashauri  hiyo mpya ya Nyang'wale kwa kutaka kutafutwa kwa njia nyingine za upatikanaji wa fedha hizo kupitia mapato yao.
PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-SENGEREMA.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana na mkazi wa Sengerema aliposimama kuwasalimia wananchi alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa kampeni. 
 Mkuu wa msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Ndugu Abdallah Bulembo akitoe maeleoz mafupi kwa wakazi wa Nyang'wale namna ya kuwapigia kura wagonbea wa CCM. 

Mgombe Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiwanadi madiwani wa wilaya ya Sengerema mbele ya maelfu ya wananchi alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni,ambapo aliwaomba wampigie kura za kutosha ili aibuke mshindi na kuwa rais wa awamu ya tano
 Wakazi wa mji wa Sengerema wakimsikiliza Mgombe Urais wa CCM Dkt John Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni,ambapo aliwaomba wampigie kura za kutosha ili aibuke mshindi na kuwa rais wa awamu ya tano.
  Wananchi wakiwa wamefunga njia wakitaka Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli awasalimie na pia wamweleze shida zao,ili iwapo akichaguliwa katika nafasi ya Urais baasi aweze kuwakumbuka na kuwasaidia.
Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiingia kwenye kivuko cha Mv Misungwi katika feri ya Busisi akitokea wilayani Sengengerema kuelekea jijini Mwanza baada ya kumaliza mikutano yake ya kampeni aliofanya katika wilaya ya Geita vijijini,wilaya ya Nyang'wale pamoja na Sengerema mkoani Mwanza.
 Wakazi wa mji wa Sengerema wakishangilia ujio wa Dkt Magufuli alipokuwa akipita mjini Sengerema kuelekea jijini Mwanza.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya  Sengerema kwenye mkutano wa kampeni 
 Wananchi wa Sengerema wakimsikiliza Mweyekiti wa chama cha CCM mkoa wa Mwanza,Ndugu Anthony Dialo,alipokuwa akimkaribisha kiongozi wa msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Ndugu Abdallah Bulembo ili amkaribishe mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli awahutubie Wananchi.
 Maelfu ya wananchi wa Sengerema wakifuatilia mkutano wa kampeni.
 Wananchi wakiwa wamefunga njia wakitaka Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli awasalimie na pia wamweleze shida zao,ili iwapo akichaguliwa katika nafasi ya Urais baasi aweze kuwakumbuka na kuwasaidia.

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya mpya ya Nyang'wale,katika uwanja wa shule ya msingi ya Jitundu,kwenye mkutano wa kampeni.
 Vijana na Mabango yao
 Wanachi wa Sengerema wakishangilia msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akipita kuendelea na mikutano yake ya kampeni.
Next Post Previous Post
Bukobawadau