Bukobawadau

PITIA SIMULIZI; I LOVE YOU!!! (NAKUPENDA)

 Mwezi mmoja baada ya kumaliza elimu yangu ya kidato cha sita 2009 February 12 huko jijini Mwanza nilirejea nyumbani kwetu Mbeya.......
Nyumbani kwetu nipakawaida sanaa lakini nashukuru Mungu tulikuwa tunauwezo wa kupata chakula (asubuhi, mchana na jioni)
Nakumbuka siku moja niliwahi kusikia baba yangu akizungumzia kuhusu swala la kuwasaidia yatima.. Wajane pia kuwatembelea wafungwa.......
Nilibahatika kupata kakazi ka kufundisha shule moja pale mtaani kwetu jambo ambalo liliniwezesha kupata hela kidogo ya kujikim..... Baada ya kulipwa niliwanunulia wazazi wangu zawadi japokuwa ilikuwa ndogo ***** siku hiyo jioni wakati wa Sala mama yangu aliniita faragha na kuniuliza '' mwanangu Mau hivi toka uzaliwe ushaawahi kwenda kuwatembelea watoto yatima? '' nilimjibu mama kwamba sijawahi...... Mama akaniambia basi siku moja jipange twende tukawatembelee '' lakini mama kwa kitu gani hasaa tulichonacho ili tuwatembelee '' nilimjibu mama yangu......... Mama alizidi kunielewesha kwamba chochote ukitoa kwa Moyo basi hicho ni kikubwa sanaaa kwa Mungu......... Tulizidi kuongea sana hatimae tulifikia muafaka kwamba jumapili tungeondoka......
Jumapili majira ya saa saba tulianza safari yetu mimi, baba na mama....
Tulifika salama na tulipokewa vizur sanaa na mda wa kukutana na watoto pamoja na kuwapa chochote kitu ulifika...............
 Ilikuwa ni ngumu sanaa kwangu pale ambapo mtoto mmoja alikuja moja kwa moja kwangu....
Mtoto huyu alikuwa kati ya miaka 6 mpaka 7 (Maurine) alipokuja alinirukia '' baba shikamoo.. Kwanini umeniacha hapa??? Leo si tutaondoka wote?? '' Maurine alizidi kuongea huku analia na mimi nililia pia kwa sababu ni wazi kwamba Sina mtoto lakini nilijua fika mtoto yule anamis mapenzi ya wazazi wake na wengine wapo pale hawajui kwamba wazazi wao hawapo tena duniani..........
Kiukweli nililia sanaa baada ya kuona machozi ya binti huyu lakini nililia zaidi kwa kuwa mimi sio baba yake japo sikuweza kamwambia ukweli....... Tulizidi kupiga story na maswali yake mda wote yalikuwa magumu kwangu '' baba leo si tutaondoka wote?? Naomba usiniache!!! Nilimwambia nakupenda na sikuachi ***** niliendelea na kuwasalimia watoto wengine lakini Maurine tulipokuwa tunapita aliwaambia watoto wote kuwa mimi ni baba yake na aliwasisitizia kuwa tunaondoka wote!! Upande wa pili nilimuona baba yangu na mama wakiwa wanafurahi pamoja na watoto wengine.... Walipiga picha kadhaa na mimi pia nilijumuika nao..........
Mda ulisonga mbele hatimae muda wa kuondoka uliwadia na watoto waliambiwa warudi ndani kwenda kuoga....... Ulikuwa ni muda mgumu zaidi kwangu Maurine alilia sanaa kitendo cha mimi kuonyesha ishara za kumuacha 😭😭 nilimpa tsh 10000 nikamwambia '' nakupenda sana mwanangu basi nenda ukaoge uje twende '' na niliahidi nafsi yangu kwamba ningekuja tena siku nyingine......... Nlimuachia namba yangu ya simu lakini pia anuani yangu.......... Aliondoka akiwa anaamini kwamba atanikuta pale pale 😭😭......
Mara baada ya kuondoka Maurine safari yetu ilianza lakini roho yangu ilifadhaika sanaaa mda wote hususani nikiyakumbuka Yale maneno............... Mwezi mmoja badae baada ya kupata kale kamshahara kangu nilifunga tena safari kwenda kumuona Maurine........
Nilifika kule na nlipokelewa vizuri sanaaa... Muda kidogo baadae nililetewa barua ya Maurine ambayo ilikutwa kwenye begi Lake..... Sister walinipa taarifa kwamba Maurine alipotea siku moja baadae akiwa ananitafuta mimi. 😭😭😭😭............. Walitoa taarifa polisi lakini mafanikio yalikuwa F..... Hatimae siku nne baadae kadri ya maelezo ya sister mwili wa Maurine ulipatikana ukiwa umeharibika sanaaa (amekufa) nililia sanaaaa
Nilikubaliana na Ile hali ndipo nikaamau kusoma Ile barua ya Maurine '' NAKUPENDA SANA BABA.... KWA NINI UMENIACHA?................ ........!''Barua Ile ilikuwa ndefu japo hati yake ilikuwa bado ya kitoto ila niliielewa sana,,,,,,,,,,, sikuamini kwamba niliyoyasikia ni kweli ama ndoto............. 😭😭😭😭😭😭😭 won't forget you Maurine...... Huenda ndicho kifo chako ulichopangiwa ila naumia kwamba umekufa ukiwa unaamini mimi ni baba yako 😭😭..............
Story hii ni ya kweli ila tu nimebadilisha baadhi ya majina kwa makusudi maalum...........
 Nimesukumwa kuandika haya baada ya kuona kwamba wengi tupo tayari kuchangia anasa kama vile graduation lakini mambo ya kusaidia wahitaji kama
Wajane
Yatima
Wafungwa
Wagonjwa nk.
Tumeachana nayo ila kuchangia vitu vingine tupo tayari ili yule na yule wakuone na upewe sifa (papaa fulani)........wewe unachangia nini zaidi..tafakari chukua hatua.
Next Post Previous Post
Bukobawadau