Bukobawadau

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU DEC 24,2015

 Camera yetu mtaani leo Alhamis Dec 24,2015 inakutana na wadau waishio Jijini Dar,kutoka kushoto ni Bwana Tbs, Mr Ben Mulokozi aka Mr.appetizer (Binuzi) na Ndugu Ruta Rwabigene wakiwa tayari kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya nyumbani
 Taswira  mjini kati
 Wadau kama walivyokutwa na Camera yetu wakibadilishana mawazo, hapa na maeneo ya Mtk kwa Dada Jane ajenda kubwa ni lile tamasha lililoandaliwa na Mbunge maarufu kama tamasha la BUMUDECO ambalo litakuwa Jukwaa la kila mwaka la kuwakutanisha wadau wote wenye maslahi na kiu ya dhati ya kuiona Bukoba ikipiga hatua za kimaendeleo kwa kasi inayostahili
 Mtaalam mwemezi kimasha pic kushoto akiwa tayari mjini hapa kwa ajili ya kushiriki lile tamasha la Bumudeco
 Hekaheka za hapa na pale mbele ya lango la Soko kuu Mjini Bukoba
 Bwana TBC akiteta jambo na Dada Jane wa MTK Miembeni
 Kutoka Jijijini Dar pichani ni ndugu wa familia ya Marehemu mzee Kahwa,muda mchache kabla ya kuelekea Kijijini Kanyigo kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya

 Mdau Ruta Rwabigene katika Ubora wake.
Mdau mpambanaji Bushira mbele ya Camera yetu.


MWALIKO WA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIMAENDELEO—MANISPAA YA BUKOBA
JUMAPILI, TAREHE 27/12/2015 KUANZIA SAA 10:30 JIONI KATIKA UKUMBI WA ST. THEREZA

1.      UTANGULIZI
Mbuge wa Bukoba Mjini akishirikiana na Balaza la Madiwani na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba wanapenda kuwakaribisha wale wote wenye maslahi na maendeleo ya Manispaa ya Bukoba; ambayo ni sebule ya mkoa wa Kagera, kwenye Kongamano la Kimaendeleo litakalofahamika kama BUKOBA MUNICIPAL DEVELOPMENTAL CONFERENCE (BUMUDECO). Kongamano hili litafanyika Jumapili, Tarehe 27/12/2015 kuanzia Saa 10:30 Jioni Mjini Bukoba katika ukumbi wa St. Theresa. Mpaka sasa watu wa nafasi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Kagera, nchi jirani na nchi za mbali wameonyesha nia ya kutumia likizo zao za mwisho wa mwaka kushiriki nasi Mkutano huu.

BUMUDECO litakuwa Jukwaa la kila mwaka la kuwakutanisha wadau wote wenye maslahi na kiu ya dhati ya kuiona Bukoba ikipiga hatua za kimaendeleo kwa kasi inayostahili. Katika mkutano wake wa kwanza BUMUDECO inapanga kuwa na shughuli zifuatazo:

·         Kuwasilisha Mpango-Kazi wa Mbunge na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa  Bukoba kwa kipindi cha mwaka 2015-2020 ikiwa ni tafsiri ya yale walioahidi katika kipindi cha kuomba kura. 
·         Kubainisha fursa za kibiashara, uchumi na maendeleo zinazopatikana ndani ya Manispaa na vivutio vitakavyotolewa na uongozi mpya kuvutia na kuhamasisha uwekezaji.
·          Kuthibitisha utayari wa uongozi mpya wa kisiasa na watendaji wa Manispaa katika kushirikiana na wadau kuondoa mkwamo wa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa
·         Kupokea mada na Michango mahususi kutoka kwa wanataaluma, wawekezaji na wajasiriamali mbalimbali kwa ajili ya kupeana ufahamu na uzoefu.
·         Kuanzisha na kujenga Jukwaa la wadau wa Maendeleo ya Manispaa ya Bukoba kwa ajili ya kujenga mshikamano wa pamoja, kufahamiana na kuweka utaratibu wa kukutana walau mara moja kila mwaka.
·         Kutoa fursa kwa wadau wa ndani na nje ya Bukoba kufurahi pamoja, kuburudika na kusherehekea mafanikio walioyapata katika shughuli zao kwa mwaka 2015

Pamoja na mwaliko huu, BUMUDECO inakaribisha wadau kuonyesha nia  (Expression of Interest) katika kuanzisha na kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kimaendeleo ndani ya Manispaa ya Bukoba.

2.      SEHEMU KUU ZA BUMUDECO 2015
2.1        MKUTANO
Hii itakuwa sehemu ya kwanza ya tukio la BUMUDECO  itakayoanza saa11:00 Jioni na kuhitimishwa saa 2:00 usiku. Katika sehemu hii wageni waalikwa na viongozi nbalimbali watambulishwa na kutoa salamu. Shughuli kuu katika sehemu hii itakuwa uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizoandaliwa na Wataalam pamoja na wawakilishi wa makundi ya Jamii. Washiriki wa ndani na nje ya ukumbi watapata fursa kuchangia mijadala na kila mada itatamatishwa kwa maazimio yatakayotekelezwa. Taratibu zinafanyika ili kwa kutumia TEHAMA, wadau watakaoshindwa kushiriki moja kwa moja ukumbini waweze kushiriki kupitia matukio yatakayo rushwa moja kwa moja kupitia Mtandao.

Mada na watoa mada watakaowasirisha mada ni hawa wafuataio:

S/No.
Mtoa Mada
Mada
1         
Leopard Rweyemamu
Fursa za Uwekezaji na Utayari wa Manispaa ya Bukoba Kufanikisha Miradi ya Maendeleo
2         
Ali Mufuruki
Umuhimu wa Taasisi za Kifedha na Jitihada za Wadau wa Kagera
3         
Anic Kashasha
Ushawishi kwa Wawekezaji na  Hatua za Mafanikio—Mtazamo wa Sekta Binafsi
4         
Prof. Lwaitama
Historia ya Mafanikio ya Elimu Mkoani Kagera; Tunarejeaje Kileleni?
5         
William O. Rutta
Nafasi ya Utalii katika Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera; Fursa na Changamoto
6         
Jamal Malinzi
Michezo kama Uwekezaji na Ajira; Nini Fursa za Kagera?  
7         
John G. Ndibalema
Mchango wa Vijana katika Kagera ya Leo na Kesho

2.2        SHEREHE
Baada ya saa 2:30 usiku, mara tu baada ya mkutano kufungwa, mpangilio wa ukumbi utabadilishwa na maeneo ya wazi katika viwanja vya St. Thereza vitatumika kwa sehemu ya pili ya tukio la BUMUDECO ambayo itakuwa Sherehe yenye maudhui ya kufahamiana na kupongezana kwa yote ambayo Mungu amejalia kuyafanikisha katika mwaka wa 2015. Washiriki watapewa nafasi ya kuchanganyika, kuzungumza, kubadilisha mawasiliano huku wakipata burudani, vinywaji na chakula. Kwa kiwango cha kutosha viburudisho katika sherehe hii vitalenga kudhihirisha utajiri wa tamaduni za Mhaya lakini pasipo kuwapunja wale wanaopenda radha tofauti.



3.      KUSHIRIKI
Mpaka dakika hii, Kamati imefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha malengo ya BUMUDECO 2015 yanatimia na kila mdau anaridhika kwa muda na rasilimali zake atakazozitenga ili kushiriki tukio hili. Kwa kuzingatia matarajio, maoni na mapendekezo ya wadau, Kamati imeridhia pendekezo la TZS 50,000/= (Elfu hamsini) kama ada ya uanachama wa kujiunga na BUMUDECO. Kwa ada hii, pamoja na kutambulika rasmi kama mwanachama kwa mwaka mzima, mdau atapata tiketi ya kushiriki mkutano wa BUMUDECO 2015, atahudhuria sherehe na atapewa huduma zote za vinywaji, chakula na burudani. Pia wadau wote watakaoshiriki BUMUDECO 2015 wataingizwa kwenye kanzidata yakupewa Taarifa za Mkutano na maendeleo ya utekelezaji wa maazimio ya mkutano.

3.1        JINSI YA KULIPIA NA KUPATA KADI
Kadi zinapatikana Bukoba Mjini katika vituo vifuatavyo:

·         Uswahili Manyema CafĂ©
·         Total Petrol Station
·         Ofisi ya Meya wa Manispaa
·         Ofisi ya Mbunge Bukoba
·         Ofisi ya Mkurugenzi

Pia Kamati imesajili namba maalumu za mitandao mitatu kumsaidia mshiriki kutuma ada yake. Kupata tiketi yako tuma TZS 50,000/= kwenye moja ya namba zifuatazo:

·         M-Pesa 0743-059-595;
·         Airtel  Money 0785-311-884; 
·         tiGo-Pesa 0717-656-769

NAMBA ZOTE ZINASOMEKA JINA: BUMUDECO BUKOBA. Pesa yako itakapopokelewa utapigiwa simu na Mwanakamati atakayechukua majina yako kamili na kukupatia neno-siri/nywila utakayotumia kuingia kushiriki BUMUDECO 2015.  


KARIBU NYOTE/MUNYEGERE WAITU!

Imetolewa na Kamati ya Maandalizi
Next Post Previous Post
Bukobawadau