Bukobawadau

MSAADA MKUBWA UNAHITAJIKA KWA DADA ELIZA ILI AWEZE KUFANYIWA UPASUAJI WA UVIMBE TUMBONI

Eliza Juma (30), mkazi wa Mtaa wa Mbwanga Manispaa ya Dodoma anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa yeyote ataeguswa ili aweze kufanyiwa upasuaji wa uvimbe tumboni ambao umekuwa ukiongezeka kila siku.

Akizunguma na waandishi wa habari mjini hapa Dodoma, alisema kuwa uvimbe huo ambao umekuwa ukiongezeka kila siku umekuwa kikwazo kwake katika kutekeleza majukumu yake ya kujipatia kipato.

Alisema kuwa uvumbe huo unaotokana na yeye kufanyiwa upasuaji wa utumbo aliofanyiwa miaka miwili iliyopita kutokana na utumbo wake kujikunja.

“Nilifanyiwa upasuaji wa utumbo miaka miwili iliyopita katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambapo utumbo wangu ulikuwa umejikunja lakini mara baada ya kufanyiwa upasujai huo kidonda kilianza kuwasha na mimi nikawa napakuna ndipo pakaanza kuvimba hadi kufikia ukubwa huu unaouona sasa” alisema Eliza.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo alikwenda hopitali ya mkoa ili kuweza kuonana na daktali ambaye alimweleza kuwa tatizo hilo linatokana na ngozi ya ndani kulika hivyo anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine.

Aidha alisema kuwa kutokanana hali yake ya kiuchumi na kiasi alicho ambiwa kulipia ili awze kufanyiwa upasuaji huo yeye hawezi kumudu kwakuwa hana msaada wowote anaoutegemea zaidi ya wasamailia wema.

“Kiasi kinacho hitajika ili niweze kufanyiwa upasuaji ni zaidi ya shilingi laki tatu na mie kama mnavyo  hapa nilipo natunzwa na wasamilia wema sina mama wala baba hivyo nawaomba wasamalia wema kunisadia ili niweze kupata kiasi hicho kwaajili ya matibabu kabla tatizo halijawa kubwa zaidi”alisema Eliza.

Alisema kuwa kwa yeyote atakaye guswa anaweza kumchangia anaweza kuwasiliana naye kupitia namba ya simu ya mkononi 0678164633 ili aweze kupata kiasi hicho cha pesa na kupatiwa matibabu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau