Sehemu ya wizi wa maji kutoka katika mtandao wa DAWASCO unavyoone3kana kufanywa katika kiwanda cha kutengenezea Betri cha Bahari Chemicals Ltd.
Ikiwa
siku chache tu zimepita baada ya shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam
(Dawasco) kubaini wizi mkubwa wa Maji kutumika katika shamba la mboga mboga na
matunda katika chuo cha Islamic kilichopo Boko ununio jijini Dar es salaam.
Dawasco imebaini wizi mwingine wa Maji katika kiwanda cha kutengeneza Maji ya
betri cha Bahari Chemicals Ltd kilichopo kurasini wilaya ya Temeke jijini Dar
es salaam.
Akizungumzia
tukio hilo meneja wa Dawasco Temeke, Bw. Deogratius Rwegasira, amethibitisha
kutokea kwa wizi huo ambapo kiwanda hicho kilikuwa kimejiunganishia Maji bila
kibali cha Dawasco na kwamba hawakuwa na mita wala akaunti namba inayoonyesha
kiasi cha Maji kinachopita katika system ya Maji iliyopo, na baada ya kufanya
mawasiliano na Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Devendra Singh Parmar amekiri
kutumia Maji hayo kinyume na taratibu .
“Baada
ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa kiwanda hiki kimekuwa kikituibia Maji yetu
kwa muda mrefu, mmiliki wa kiwanda amekubali kosa,lakini akisema kwamba wenyewe
ni wageni hapa hawana zaidi ya mwaka mmoja tangu waanze kazi.hivyo hawakujua
taratibu za kufuata”. Alisema Bw. Rwegasira.
Aidha
meneja wa kiwanda hicho, Bw. Abdul Gulam, amekiri kuihujumu Dawasco kwa kuiibia
Maji, lakini amesema kuwa wao ni wapangaji tu wamepanga katika eneo hilo na
wana muda wa miezi saba tangu wahamie kiwandani hapo, walikuta wizi huo wa Maji
ukifanyika katika kiwanda hicho na
hawakujua taratibu husika za kufuata ili wapate huduma ya Maji kihalali.
“Sisi
tumekubali kuwa tulikuwa tunatumia Maji ya DAWASCO bila kuyalipia, lakini sio
sisi ambao tuliounganisha bomba hili, wapangaji waliopita walijiunganishia Maji
haya hivyo tunaomba tulimalize hili, ili tuanze kuwa wateja wenu rasmi” alisema
Bw.Gulam.
Aidha
bwn Gulam ameainisha kuwa wao kama wamiliki wa kiwanda wamekubali kulipa faini
iliyotolewa na DAWASCO ya Shiling million 3.5 ili warudishiwe huduma kama
wateja wengine na waweze kuendelea na biashara.
Vitendo
vya uhujumu wa Miundombinu ya Maji hususani wizi wa Maji unaendelea kuwa
changamoto kwa DAWASCO licha ya kampeni na elimu inayotolewa kila siku juu ya
uhalali na utaratibu wa kuungiwa huduma ya Maji inayotolewa na DAWASCO.
Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.
|