Bukobawadau

KASHOZI ROAD BUKOBA LEO JAN 21,2016

@Kashozi road Bukoba ;Hii ni moja kati ya barabara mbili (2) kuu zinazotoka na kuingia katika mji wa bukoba.
Barabara hii ina upana wa kadirio la mita 9.8 na hutumika kwa vyombo vyote kama pikipiki, baiskel, magari makubwa na madogo. Lakini pia hutumika kwa waendao kwa miguu. Ni barabara ambayo iko busy sana wakati wote, zaidi asubuhi na jioni.

Pia kuna shughuli mbali mbali za kiuchumi zinafanyika pembezoni mwa barabara hii zikiwemo rasmi na zisizo rasmi mfano ofisi mbali mbali kama Mayawa, Sido, vituo vya mafuta, maduka, mitumba, salon, magenge, pikipiki, biashara za kushika mkononi n.k. Katika barabara hii pia kuna makazi ya watu ambayo yamejengwa mita 2 kutoka eneo la barabara
Barabara hii imeonekana kuwa finyu hasa kutokana na kufungwa kwa barabara ya Miembeni-Kashai kutokana na upanuzi wa uwanja wa ndege na msongamano wa watu hususani maeneo ya Kashai, Nyamkazi, Katatorwansi, Mafumbo hadi Kisindi.
Pia ukanda wa barabara hii una shule nyingi zaidi za sekondari na msingi, vyuo vikuu kama JoKUCo, Chuo Kikuu Huria na King Rumanyika.
Na ni ukanda ambao biashara ya mazao ya ziwa, parachichi, mutwishi na fia kati ya Bugabo na mjini yameshamiri, bila kusahau biashara na uvuvi pia katika maeneo kama Nyamkazi na Musila.

Kwa ongezeko la idadi ya watu kwa wastani wa 2.7% sawa na takwimu za sensa ya 2012, na sababu nyingine tajwa hapo juu, barabara hii itazidi kuwa finyu na pengine kusababisha foleni kubwa sana na pengine ajali siku za mbeleni.
Hivyo ni vyema kuangaliwa kwa jicho la tatu, na mkakati maalumu wa upanuzi kuanza utakaozingatia kuweka sehemu ya kupita watumiaji wa baiskeli na pikipik, sehemu ya kupita magari na waendao kwa miguu. Na pia kufungua njia nyingine mbadala zinazounganisha maeneo flani kama Nshambya na hamugembe, kyabitembe ,Rwamishenye na kwingineko

VIA Bukobawadau Entertainment Media

BUKOBA - Kazi, Amani na Maendeleo
 NDUGU MSOMAJI NI NINI MAONI YAKO JUU YA HILI?
Next Post Previous Post
Bukobawadau