MAONESHO YA BIASHARA YA ESTHER LAND SHOW AFRIKA KUSINI YAVUTIA WAFANYABIASHARA WENGI ZAIDI KUTOKA TANZANIA
Na EmanuelMadafa,Mbeya,Mbeya
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Afrika kusini (Esther Land Show) ambayo hufanyika kila mwaka nchini humo yameendelea kuvutia wafanyabiashara wengi zaidi kutoka nchini Tanzania.
Pia Maonesho hayo hufanyika katika mji wa Johnsburg ambapo kwa mwaka huu yanatalaji kuanzia Mwezi Machi 23 hadi April 03 mwaka huu huku idadi ya wafanyabiasahara hao waliojitokeza imetajwa kufikia zaidi ya watu 100 ,hasa kutoka katika mikoa ya Kanda ya Ntanda za juu kusini.
Katika kufanikisha safari ya wafanyabiashara hao kampuni ya Blue Bird Buleau De
Change iliyopo Jijini Mbeya imeamua kudhamini safari hiyo kwa kutoa usafiri wa kwenda na kurudi kwa
basi la Twiga Intarnational ambapo kila mfanyabiashara atachangia kiasi cha shilingi laki nne na nusu (450000).
Akizungumza jijini mbeya, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Jankey
Ndingo, amesema ziara hiyo imelenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania
na nchi ya Afrika ya kusini katika kujengeana uwezo ikiwa na kutangaza fursa
zilizomo kwenye maeneo yao.
“Mji wa Johnsburg umekuwa ukiendesha maonesho ya biashara kila
mwaka katika Sikukuu ya Pasaka, hivyo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa
wakihudhuria maonesho haya lakini kwa mwaka huu tunataka kuwashirikisha
wafanyabiashara wadogo ili nao wafike na kunufaika na fursa hiyo,”alisema.
Amesema, maonesho hayo yamejikita zaidi katika masuala ya matumizi
ya mitambo mbalimbali kama vile mitambo ya kilimo,vifungashio pamoja na ile
inayozalisha bidhaa zikiwa na kiwango cha ubora unaoendana na soko la
kimataifa.
Amesema, Afrika kusini kumekuwa na soko kubwa la bidhaa za
kitamudi na zao la tangawizi zinazozalishwa Tanzania hivyo ni vema
wafanyabiashara wakatumia fursa hiyo kwenda kutafuta masoko na kuanza
kusafirisha bidhaa hizo.
“kinachotakiwa kufanywa na wazalishaji ni kuhakikisha bidhaa zote
zinakidhi kiwango cha ubora wa kimataifa,”alisema.
Aidha, amesema kuwa ziara hiyo inashirikisha wafanyabiashara wote
wanaonesha nia ya kutaka kujifunza na kubadilika ili kuondoka na hali ya
umaskini na kwamba safari hiyo itaanzia Mjini Mbeya kwa usafiri wa basi
kupitia njia ya Zambia na kwa gharama nafuu.
Hata hivyo, amesema kuwa safari hiyo itakuwa ni ya kitalii zaidi
kwani wafanyabiashara watapata fursa ya kutembelea maporomoko ya mto Zambezi
yajulikanayo kama Victoria yaliyopo nchini Zambia na kwamba ziara hiyo itakuwa
ya siku 13.
Mwisho.
Jamiimojablog
Jamiimojablog