Bukobawadau

KAMPUNI YA MAWASILIANO YA TIGO YATOA MSAADA WA FEDHA ,KIASI CHA SHILINGI MIL TANO NA VIFAA VYA MICHEZO KWA WATOTO WA KITUO CHA AMANI CENTER CHA MJINI MOSHI.

Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kanda ya Kaskazini,Henry Kinabo (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 5 afisa uhusiano wa kituo cha kulea watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Amani Center ,Kampuni ya Tigo imetoa kiasi hicho cha fedha pamoja na vifaa vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya mbio za Kilimanjaro Marathoni.
Meneja wa kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini,Henry Kinabo akikabidhi fulana kwa watoto waishio katika mazingira magumu ya Kituo cha Aman Center cha mjini Moshi.
Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini ,Henry Kinabo akifurahia jambo na afisa uhusiano wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Amani Center ,Salma Khatibu,wengine ni watoto waishio katika kituo hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau