Bukobawadau

PUNGUZO LA BEI KUTOKA SHIRIKA LA NDEGE LA RWANDAIR

Meneja Mkazi wa Shirika la Ndege la RwandAir, Ndugu Ibrahim Bukenya akiwa ofisini kwake.
 Shirika la Ndege la RwandAir limetangaza kuwepo kwa punguzo la bei zake kwa kuelekea sehemu zifuatazo: Kigali, Nairobi, Mombasa, Entebbe, Bujumbura, Kamembe, Lusaka, Johannesburg, Dubai, Accra, Lagos, Douala, Juba, Libreville, Brazzaville. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkazi wa Shirika hilo, Ibrahim Bukenya amesema wameamua kutoa punguzo hilo ili kuwawezesha wateja wao kusafiri katika maeneo hayo tajwa kadri wawezavyo na kwa gharama nafuu. Pia amesema kwa sasa Shirika hilo lina Ndege kubwa nane 8 na linataraji kuongeza Ndege mpya mbili aina ya Airbus A330-300 na mbili aina ya Boeing 737-800 kufikisha jumla ya Ndege kumi na mbili 12, kufikia mwisho wa mwaka huu. Shirika la Ndege la Rwanda litaanzisha safari zake mpya kuelekea, Guangzhou,Lilongwe,Cotonou, Khartoum, Paris,London, Harare na Mumbai na kufanya jumla ya safari zake kuwa 23. 
 Bwana Bukenya wa pili kutoka kulia pichani ameongeza kwa kusema kuwa niwakati sasa kwa Mtanzania kutumia Shirika la RwandAir kwani wako na bei nafuu, Kusafiri kwa raha na Ndege mpya, Kupata huduma bora kuanzia wakati wa kupata tiketi hadi mwisho wa safari. Kwa huduma zaidi tembelea wakala wa RwandAir aliyeko jirani yako au nenda ofisi zao zilizoko jengo la Viva Towers ghorofa ya pili na unaweza kuwapata kwa namba za simu 0782 039152 au 022 2103435 na barua pepe sales.dar@rwandair.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau