Bukobawadau

BARAZA KUU CHADEMA:Katibu Mkuu wa CHADEMA ni Dkt. Vicent Mashinji.

#‎BarazaKuuCHADEMA‬ "Suala ambalo hatutalivumilia ndani ya Chama ni suala la rushwa, linagawa taifa" M/kiti Mbowe. Mabadiliko daima.
 #‎BarazaKuuCHADEMA‬ "Tumetafakari,kama CCM wameshindwa kutatua tatizo la ajira kwa vijana, sisi Chadema tunafanyaje? M/kiti Mbowe. Mabadiliko daima.
 Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vicent Mashinji akiwa anatoa shukrani na nasaa muda mfupi baada ya uteuzi. ‪#‎BarazaKuuChadema‬
 #‎BarazaKuuCHADEMA‬ Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akihutubia mkutano wa Baraza Kuu, leo Jumamosi 12/3/2016 jijini Mwanza.
 #‎BarazaKuuCHADEMA‬ - Mwalimu Nyerere alishawahi kusema "Duniani kuna viongozi wa aina mbili 1. Viongozi wenye upeo wa maono (Vision). 2. Na viongozi ambao kazi yao ni kutunza hesabu, nimepewa kiasi hiki nimetumia kiasi hiki ndo kazi yake, athubutu haoni mbali, viongozi wa aina ya pili ndio wengi Afrika wanaofanya book keeping, IMF imwambia nini, tekeleza hili tekeleza hili, viongozi hawa hawatuvushi, tunataka viongozi wa kutuvusha, kiongozi mwenye vision" Mhe Edward Ngoyai Lowassa. Mabadiliko daima.
 #‎BarazaKuuCHADEMA‬ - Baadhi ya Wajumbe wakionekana kwenye picha kutoka ukumbini jijini Mwanza. Mabadiliko daima.
 Viongozi wa Chama wakiongozwa na M/kiti. Freeman Mbowe, wakiwapungia wajumbe wa Baraza Kuu leo Machi 12/2016, jijini Mwanza. Mabadiliko daima.

Next Post Previous Post
Bukobawadau