Tunakushukuru Eh Mungu kwa kutulinda usiku kucha na kutuwezesha kuamka salama Jumanne hii ya leo. Tunaomba uzidi kutulinda na kutuongoza katika kila jambo siku zote za maisha yetu.
Mtakatifu Mungu tunaomba heri na baraka maishani mwetu na katika maisha ya familia zetu kwa ujumla. Utubariki katika kazi zetu, biashara na katika kila njia halali ya kujipatia kipato ili kwamba sote tupate kufanikiwa kwa kadri ya mapenzi yako.
Tunaomba utuepushe na magonjwa na matatizo ya kidunia; utujalie afya njema na baraka tele. Utupe busara na hekima ya kutambua mema na mabaya na pia utupe nguvu za kuyashinda majaribu ya kidunia ili kwamba tuweze kuishi kwa namna ya kukupendeza.
Tunaomba haya yote tukiamini na kusema.
0 comment:
Post a Comment