Bukobawadau

MINZIRO-MISSENYI :BALOZI DR KAMALA AITIMISHA ZIARA YAKE JIMBONI MWAKE

 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akipokelewa na Viongozi mbalimbali wa Kijiji cha Bulembo mara baada ya kuwasili kijijini hapowasili katika Kata ya Minzoro ikiwa ni muendelezo wa ziara katika jimbo lake lenye jumla ya kata 20
 Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akamilisha ziara jimboni mwake,Madhumuni ya ziara hiyo ilikuwa ni kutoa shukrani kwa wananchi waliomchagua pamoja na kubaini kero mbalimbali zinazowakabi wananchi wate wa Jimbo la Nkenge
Pamoja na mambo mengine katika ziara hizo Balozi Dr. Kamala amechangia miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata zote 20 na kuahidi kusaidia kutatua kero za msingi zinazowakabili wananchi likiwemo swala la Maji na migogoro ya Ardhi.
Bango la Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Asili wa Minziro wenye wanyama na ndege wa aina ya mbalimbali,Msitu Uliojaa vipepeo vingi venye rangi mbalimbali,hifadhi hii ni pekee kabisa anamo patikana nyoka aina ya Cobra mwenye umri wa miaka 218 na miezi minne kufikia mwezi Jana.
Baadhi ya Wakazi wa kata ya Minziro yenye Vijiji Vitatu ambavyo ni Karagala,Minziro na Kigazi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge uliofanyika Jana March 4,2016 Katika Ofisi ya Kijiji Kigazi
Kabla ya Mkutano huo Mh Mbunge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala amepata taarifa fupi ya Shughuli za kimaendeleo katika Kata ya Minziro,taarifa inadhibitisha kuwa hali ya Chakula ni nzuri kutokana jamii kuhamasishwa kulima kilimo cha masika kwa aina zote za mazao yanayolimwa eneo hilo ikiwa ni pamoja na kila Kaya kulima hekta moja ya zao la maharage  ya njano aina ya (Uyola) ikiwa ni agizo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Missenyi.
 Pichani anaonekana Mwl. Mkuu wa Shule ya Msingi Kyanumbu iliyopo kijiji cha Kigazi-Minziro
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akiwahutumia wananchi waliohudhuria Mkutano huo pamoja na kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa wananchi,awali Mh.Balozi Kamala alitoa  Msaada wa Saruji mifuko 50 kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara na katika mkutano huu ameweza kuchangia mifuko 50 kwa ajili ya Ujenzi wa Chumba cha Darasa la awali kwa ajili ya Vijiji vya Bikunyu na Kayunga.
 Aidha Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala amewataka watendaji wa Wilaya ya Missenye kufanya zaidi kwa kujituma na kwa uzalendo wa hali ya juu kabisa kwendana na Serikali ya 'hapa kazi tu'
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kuelezea Changamoto mbalimbali alizo zibaini katika Jimbo katika Sekta ya Elimu na Afya.
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akipokea Shairi maalum kutoka kwa Wananchi wa Kijiji cha Karagala
 Wananchi wa Kijiji cha Bulembe wakimsikiliza Mbunge wao
 Ndugu Twaha Y. Lubyai, Diwani wa Kata ya Minziro akitolea jambo ufafanuzi
 Mwalimu Audax Joseph  mwalimu Mkuu wa Shele ya Sekondari Minzoro akitoa maelezo baada ya Mbunge Balozo Dr. Kamala kumtaka aeleze juu madawati 80 anayodai yalichukuliwa na DED wa Wilaya Missenye na kuyapeleka shule ya  Mabare Sekondariiliyokuwa na uwaba wa madawati kwa msingi kwamba yatarejeshwa shuleni hapo pindi yatakapo patikana ya ziada kutoka halmashauri
Balozi Dr.Kamala ameonyeshwa kukelwa na Mgogoro huo na kumtaka mwenyekiti wa halmashauri kufuatilia undani wa tatizo hilo kama kweli DED Elizaberth Kitundu alihusika na swala hilo


Muendelezo wa matukio ya picha
Baadhi ya wanahabari walio ongozana katika ziara hiyo wakibadilishana mawazo


Wananchi wakiendelea kuelezea Kero zao
 Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akipokea zawadi kutoka kwa Vikundi vya Akinana wa Kata Minziro mara baada ya kumaliza kuongea nao kuahidi kutatua kero mbalimbali
Mwisho wanaonekana wadau mara baada ya mkutano huo
Next Post Previous Post
Bukobawadau