Bukobawadau

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KATIKA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA ATOA RAI MKOA HUO KULINDWA NA WAHAMIAJI HARAMU TOKA NCHI JIRANI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa awasili Mkoani Kagera kwa ziara ya siku tatu kuanzia  Machi 13 hadi 15, 2016 katika Manispaa ya Bukoba, Wilaya za Missenyi, Karagwe na Ngara.
Akitaja malengo ya ziara yake mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera alisema lengo kuu la ziara yake ni kwenda katika ranchi za Missenyi  na Kitengule Wilayani Karagwe ili kujionea zinafanyaje kazi na kuona jinsi  ya kutatua changamoto mbalimbali ili kuwepo ufugaji bora na kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima.

 Lengo la pili la ziara ya Mhe. Majaliwa alisema ni kutembelea  Gereza la Mwisa Wilayani Karagwe na Ngara ili kujionea maendeleo ya wakimbizi wafungwa wanajeshi walioletwa na Serikali katika Magereza hayo ili kuwafunza wawe raia wema  mara baada ya kubainika katika kambi ya wakimbizi iliyopo mkoani Kigoma wakiendesha mafunzo ya kijeshi kwa wenzao kambini.
Mara baada ya kusomewa taarifa ya Mkoa wa Kagera na Mkuu wa Mkoa John Mongella Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alitoa rai kwa wananchi na viongozi wa Mkoa kuhakikisha wanaulinda Mkoa ili usiingiliwe na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ikiwa ni pamoja na ardhi kutouzwa kiholela kwa wageni kutoka nje.
 Aidha, Waziri Mkuu Mhe, Majaliwa aliwaonya Wakuu wa Wilaya za Missenyi, Kyerwa na Ngara kuhakikisha wanaziba mianya ya udhaifu ilipo kwa kuingiza mifugo na uuzwaji wa ardhi holela katika Wilaya hizo huku wao wakiwepo kama vingozi wa Serikali, alisema wanatakiwa kuchukua hatua haraka sana kuziba mapungufu hayo.
Pia alitoa agizo kwa Afisa Uhamiaji wa Mkoa na Maafisa Uhamiaji wa Wilaya kuhakikisha watekeleza majukumu yao ipasavyo na kuacha mara moja tabia ya kutoa vibali hovyo vya watu kutoka nchi jiarani na kuhamia katika Mkoa wa Kagera na kuingiza mifugo pamoja na kuhozi ardhi ya wazawa.
Vilevile Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alisistiza juu ya ukusanyaji wa kodi ili Serikali iweze kuwaletea wananchi maendeleo yao. Alihoji juu ya utoroshwaji wa Madini ya bati Wilayani Kyerwa wakati viongozi wakiwepo bila kuchukua hatua. Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa alisema hali hiyo inatakiwa kukoma mara moja kutorosha madini hayo kwenda nchi jirani bila serikali kupata mapato yake.
 Uzinduzin wa Miradi
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa alitembelea na kuzindua mradi wa maji Bunena ambao ujengwa  katika Maispaa ya Bukoba kwa ufadhili wa Serikali ya Ufaransa na umekamilika kwa asilimia 98% na gharama ya mradi huo ni zaidi ya shilingi bilioni 31na unatarajiwa kukabidhiwa mwezi Aprili 2016 mara baada ya kuwa umekamilika kwa asilimia mia moja.

Pia Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alizindua kiwanda cha Maji cha Bunena Spring Water ambacho kinazalisha maji ya kunywa na kimejengwa na Kanisa Katoliki likishirikiana na wawekezaji wawili wazawa. Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha maji safi na salaama ya kunywa chupa za Mililita 600 milioni tatu kwa siku.
wazawa. Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha maji safi na salaama ya kunywa chupa za Mililita 600 milioni tatu kwa siku.
Mkutano na Watumishi wa Serikali
Waziri Mkuu  Mhe. Majaliwa pia aliongea na watumishi wa Serikali Mkoani Kagera kwa kuwa kumbusha maadili ya kazi zao kwa kusema kuwa wajibu wa mtumishi wa Serikali ni kumpokea mwananchi, kumsikiliza, na kumhudumia au kumwelekeza mahali pa kupata huduma stahili bila kinyongo au kukasirika.

“Najua kuwa watumishi wa kada mbalimbali mnaidai Serikali stahiki zenu, Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha inalipa madeni ya watumishi na kwasababu hiyo nawaombeni  watumishi msitumie kigezo hicho cha kuidai serikali kufanya fujo au kukataa kuwahudumia wananchi. Alisistiza Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa

Mkutano wa Hadhara
Akiongea na wananchi wa Manispaa ya Bukoba katika uwanja wa Uhuru pamoja na kero mbalimbali walizoziwasilisha kwake ikiwa mojawapo ni kero ya wananchi waliopimiwa viwanja 800 na hawakugawiwa viwanja hivyo, Mhe. Majaliwa alitoa muda wa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba kuwa wawe  wametafuta utatuzi wa mgogoro huo pia aliagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu  wa fedha za serikali kuja kufanya ukaguzi kuhusu viwanja hivyo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau