SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

12 April 2016

B/NEWS:Soko la Kayanga Wilayani Karagwe laungua moto


Taarifa zilizotufikia Usiku huu ni kwamba soko la mji wa KAYANGA-KARAGWE limeungua moto na kuteketeza Vibanda vyote chanzo hakijajulikana mpaka sasa .
Wananchi wameshindwa kuuzima hoto huo kwa sababu ya kutumia vifaa duni
Taarifa zinasema baada ya muda Moto umedhibitiwa ulipoanza kusambaa kwenye maduka jirani na soko hilo kwaushirikiano wa zima moto kutoka Bukoba Mjini na Kiwanda cha Sukari Kagera.
Maoni Yetu:
Haya ni masikitiko makubwa kwa viongozi wa wilaya kubwa kama hii kukosa gari la zima moto na vifaa vingine vya uokozi.Inabidi tufike sehemu serikali nayo iache kupendelea baadhi ya mikoa.Mikoa na wilaya zote zina wananchi wanaohitaji huduma sawa.
BUKOBAWADAU MEDIA tunatoa pole kwa wote walioathirika na tukio hili

0 comment:

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU