Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu
kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa
kuamkia leo.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu
Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa
mara baada ya kuanguka na
kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani (pichani kulia).
Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru
nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya
Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na
kujizolea mashabiki wengi.
Apumzike kwa AMANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment