Bukobawadau

GARI LAZAMA BAADA YA KUTELEZA KWENYE PANTONI

Watu wawili wamepoteza maisha baada ya gari walilokuwemo kuserereka wakati likiingia katika kivuko na kutumbukia baharini eneo la Kivukoni, Dar es Salaam leo. Gari hiyo aina ya Toyota Hiace ikiwa na 2. Mwili wa dereva wapatikana, na kikosi cha jeshi la zimamoto watafuta wa pili.

===================

Habari zaidi zinasema wavukaji hao walikuwa ni waombolezaji na wametoka Mkoani Morogoro kwenda msibani eneo la KIGAMBONI na walikuwa hapo tokea saa 9 za usiku na walikuwa wengi kwa idadi ianyokadiriwa kuwa ni 15 na nia yao ikiwa ni kusubiri PANTONI ya alfajiri wawahi kuvuka nayo na walipokuwa hapo (FERRY).

Walishuka katika gari waliyokuja nayo kisha Watu wawili Dereva na Mwanamke mmoja wakakodi gari nyingine aina ya Toyota Hiace ili wakishavuka tu iwasaidie kuwapeleka wote huko Msibani kisha wao ( Dereva na huyo Mwanamke ) wakaingia katika hilo gari aina ya Toyota Hiace huku wale Ndugu wengine wakikaa katika PANTONI.

Safari ilipoanza tu hiyo Saa 10 alfajiri ya kuvuka ndipo GHAFLA ile Hiace ikarudi nyuma na KUZAMA majini wakati huo PANTONI tayari imeshafika katikati ya maji. Baada ya kuona hivyo yule Dereva akafungua mlango haraka na kuruka kutoka katika Gari na kuzama Baharini huku mwanamke aliyekuwepo ndani ya gari akashindwa kufanya lolote na akazama na ile GARI.

Taarifa ziliwafikia WAOKOAJI wa ZIMAMOTO Saa 11 alfajiri ndipo wao wakawahi kufika eneo la tukio kuanza uokoaji huku wakiomba tena MSAADA wa Jeshi la Maji ( Navy ) ambapo walianza kazi ya uokoaji tokea hiyo saa 11 na ilipofika saa 3 asubuhi hii ndiyo wakauona mwili wa yule Dereva ukielea na wakautoa lakini mpaka sasa WAOKOAJI hao wanaendelea kuusaka mwili wa yule Mama

Lakini mpaka sasa hawajafanikiwa na inasemekana kuwa huenda yule mwanamke amezama na lile gari ( Hiace ) na sasa wanafanya utaratibu wa kulitafuta hilo gari chini ya maji ili tu wautoe mwili wa yule Mama ila kipingamizi kikubwa ni hali ya mawimbi kwa sasa, mkondo wa maji yale lakini kubwa zaidi kina kirefu kilichopo pale ambapo ni takribani minazi 7 mpaka 9 ukiipanga kwa kuinyoosha.
Next Post Previous Post
Bukobawadau