Bukobawadau

HABARI KWA HISANI YA VYANZO MBALIMBALI

Watuhumiwa angalau nane wa kundi la wanamgambo wa al-Shabaab walikamatwa mwishoni mwa wiki katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Msemaji wa Shirika la Usalama na upelelezi ya Taifa, Abdi Kamil Mu'allim Shukri alisema vikosi vya usalama vilifanya msako katika maeneo maalum ikiwa ni pamoja na gereji katika Hodan, Kahda, Wadajir na wilaya ya Yakshid katika mkoa wa Benadir baada ya mashambulizi ya kigaidi hivi karibuni na kuwatia mbaroni watuhumiwa.
 "Tulipata silaha na magari kutoka gereji, na watuhumiwa 8 ambao wanauhusiano na matukio ya karibuni ya kigaidi na wanahojiwa kwa sasa," Shukri alisema.
(Picha ya mktaba)
 Zaidi ya wachoraji 150 wa sanaa ya "tattoo" ambayo inahusisha kurembesha ngozi ya mwanadamu kutumia michoro ya wino walijumuika katika mji wa Kathmandu, Nepal hapo jana kwa kongamano la sita la usanii huo. Hafla hiyo ilihudhuriwa na mamia ya waraibu wa "tattoo" maarufu miongoni mwa vijana. Waliohudhuria walipata nafasi ya kipekee kuchorewa aina mbali mbali ya "tattoo" na wachoraji waliobobea kwenye sanaa hiyo.
 Mabingwa wa ligi ya Hispania, Barcelona FC wamesema kuwa mshambuliaji wao hodari Neymar atasalia kuchezea klabu hiyo hadi atakapostaafu.
Rais wa klabu hiyo Jose Bartomeu amesema kuwa watafanya mazungumzo na Neymar ili kuendeleza kandarasi yake ya sasa ambayo inatarajiwa kuisha mwaka wa 2018.
Next Post Previous Post
Bukobawadau