
Vijana pichani kama walivyokuta na Camera yetu maeneo ya Katoma wakitoka porinikuchanja kuni

Haya ndiyo maisha halisi ya ndugu zetu Vijijini ,utaratibu wa kuchanja kuni huko maporini, upo pale pale wengi wetu tumeyapitia maisha haya,Maisha ya ukikata kucha usiku,mjomba atafariki,au ukichelewa kurudi kutoka kuchanja kuni jioni,utapelekwa na majitu kwenye mbalamwezi.

Taswira Mjini Bukoba mchana wa Jumatano April 7,2016

Maeneo ya Stendi kuu ya Mabasi Mjini Bukoba.

Majira ya Saa saba Mchana, Mji wetu ukiwa umetulia

Natamani kusema laiti kama Mkoa wa Kagera tungepata mbunge mmoja tu kama Kina Zitto Kabwe kwa namna anavyo pambania kwao na kuwapenda watu wake.
Kagera ile haikua kagera bya chance bali Ilitokana na nguvu za baadhi ya watu kama Sir George Kahama,Laurean Cardinal Rugambwa na Askofu Josiah Mutabuzi Kibira ambao ni kama hawakuacha hata mwenye kunukia harufu zao.

Kipindi kile hata 'Mwalimu Nyerere' hakuogopa wanakagera Kama Nshomile tu bali aliogopa kasi yao

Hii ni hali ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbale Kata Kitobo Wilayani Missenyi licha ya Wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati hii ndiyo Shule inayoongoza kitaalum Wilayani humo

Kwa kweli hii ni changamoto hizi ndizo Ngoma 'brass band' za shule hiyo
Unaweza kutoa maoni yako juu ya nini kifanyike!!