Mjini Bukoba , hivi ndivyo yanavyowasili Magari ya Kampuni Master Drilling& Exploration Ltd wachimbaji wa Visima vya Maji,kwa ajili ya Mradi mkubwa wa Maji unao endelea katika Kata ya Gera chini ya Shirika lisilokuwa la Serikali la Jambo Bukoba. Hapa ni maeneo ya Kyakailabwa. Safari ya kuelekea Kijijini Gera hii ni barabara ya Kyakailabwa. Mr Rahym akifuatilia hatua kwa hatua. Mlima wa Katoma Wakazi wa Gera katika mapokezi ya awali mara baada ya magari ya kuchimba mradi wa maji kuwasili Kijijini hapo Katikati ya Center ya kata hii ya Gera Gari likielekea Kashabya moja kati ya Vijiji vinne vinavyounda kata ya Gera Njia panda kuelekea Kashambya Omukitoma Bugandika kuelea Gera
Changamoto ya barabara ya Kashambya Gera Hapa tayari tupo Kituo cha Afya cha Jambo Bukoba kilichopo Gera
Tayari Magari yapo eneo la tukio Jengo la Mradi wa kituo cha Afya Gera Diwani wa Kata ya Gera, Ndugu Bitegeko akibadilishana Mawazo na Mr Rahym juu ya mradi huu mkubwa kufanyika ndani ya kata ya Gera ,mradi huo wa Maji utaweza kuwanufaisha wananchi 4098 wakazi wa kata hii na wengine zaidi kutoka maeneo mbalimbali. Mkazi wa Gera akifuatilia hatua kwa hatua kila kinachojiri Ndugu Alex na Shumbu wakifuatilia kinachoendelea Maswala ya SET UP yakiendelea Kila tukio linanaswa kwa ajili ya kuweka sawa Kumbukumbu
Uchimbaji Kisiwa ukiendelea. Vumbi likitimuka ardhini kwa kasi ya ajabu
Shughuli ikiendelea chini ya Uangalizi makini kutoka kwa Mr. Rahym Sasa Alhamdulillah!! kwa hatua hii Ashukuriwe mungu wetu baba...!
Wafanyakazi wakiendelea kuwasibika Muendelezo wa Matukio Day 1.
Ndg Mahipal mfanyakazi wa Kampuni ya Uchimbaji visima vya maji ya Master Drilling& Exploration Ltd Maji yanaendelea kutoka Chini ya ardhi ikiwa ni hatua ya awali DAY 1. Anawasili eneo la tukio Mdau Paul Rwechungura Mdau Paul Rwechungura akifurahia hatua inayoendelea katika shughuli nzima ya mradi huu Day 2. Asubuhi na mapema shughuli ikiendelea hatua kwa hatua... Muendelezo wa matukio siku ya pili Jumapili April 11,2016 kuelekea hitimisho Hatua muhimu sana ya kupump maji
NEHEMA ya maji tayari imepatiana..... Maji safi meupe yakiendelea kutoka Mashuhuda wa tukio zima Day 2, pichani Mr Rahym akitolea jambo ufafanuzi kwa Mh. Diwani Bitegeko Muonekano wa Sehemu ya Kisima cha Maji.
0 comment:
Post a Comment