Bukobawadau

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA DUKA LA DAWA NA MAGHALA YA BOHARI YA DAWA (MSD), MKOA WA MBEYA

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), akihutubia wakati wa uzinduzi wa duka na ghala la Bohari ya Dawa (MSD), mkoani Mbeya leo hii. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, Profesa Idrisa Mtulia.
 Waziri Ummy akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka hilo.
 Waziri Ummy, akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu vibao viwili kama ishara ya uzinduzi wa maghala ya mkoa wa Tabora na Tanga.
Waziri Ummy (wa tatu kulia), akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Mbeya, Daud Msasi (kulia), jinsi Kanda hiyo inavyoandaa dawa na kuzisambaza.

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (mb), amezindua duka la dawa la MSD mkoani Mbeya na maghala matatu ya kisasa ya kuhifadhia dawa yaliyopo mkoani Mbeya, Tanga na Tabora.

Waziri Mwalimu, ameipongeza MSD kwa kupata maghala matatu ya kisasa pamoja uanzishwaji wa duka la Mbeya. 

Katika hatua nyingine Waziri Mwalimu amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD vibao viwili vya uzinduzi vinavyo wakilisha uzinduzi wa maghala ya Tanga na Tabora.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu amesema ghala na duka lililofunguliwa litaiwezesha MSD kupanua uwezo wake wa kuhifadhi dawa na vifaa tiba na pia kuongeza uwezo wa kusogeza huduma karibu na wanachi.

Hata hivyo, Bwanakunu ametoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa msaada wa kiwanja cha hekari tano alioutoa kwa MSD. kiwanja hicho kipo eneo la Luguruni na ambacho kitatumika kujengea ghala la kisasa la kuhifadhia dawa kwa Kanda ya Dar-es-salaam.

Pia amemuhakikishia Rais kwamba, pamoja na msaada huu wa kiwanja na kwakuwa MSD inamahusiano mazuri na wadau wake wa maendeleo, kwasasa ipo kwenye mazungumzo ili ujenzi wa ghala la Dar-es-salaam uanze mapema iwezekanavyo na ikiwezekana mwezi Julai 2016. Kukamilika kwa ujezi huo utapunguza kiasi kikubwa cha fedha kinacholipwa kila mwaka kama kodi ya pango.

Next Post Previous Post
Bukobawadau