Bukobawadau

MADUKA YATAKAYOTOA HUDUMA YA KUUZA SUKARI !Serikali mkoani Kagera imesitisha uuzwaji wa sukari kwa biashara ya jumla, badala yake imetenga maduka maalumu kwa kila kata yatakayohusika kuwauzia wananchi sukari kwa bei elekezi ya Serikali,lengo likiwa ni kuondoa uhaba wa sukari na kuwaondolea kero wananchi.
Kwa mujibu wa Afisa Biashara mkoani hapa Isaya Tendega,uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kubaini kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya jumla wanaotumia changamoto ya upungufu wa sukari na kuiuza kwa bei ya juu tofauti na bei iliyoelekezwa na Serikali.
Tendega amesema kuwa hali ya Sukari iliyoko katika kiwanda cha kuzalisha Sukari cha Kagera ni yakutoshereza kwa wananchi wa mkoa wa Kagera,ingawa changamoto ya kuwepo uhaba wa Sukari inachangiwa kwa kiwango kikubwa kwa Wafanyabiashara kutoka nje ya mkoa kufika Bukoba kuchukua Sukari kwa bei yeyote wanayoitaka wao na kuufanya mkoa kukabiliwa na changamoto hiyo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau