Bukobawadau

'Nyakijoga' Kituo cha Hija cha Parokia ya Mugana

Kituo hiki kilianza mwaka 1954 kama kituo cha Hija cha Parokia ya Mugana.
Wakati huo Parokia ya Mugana ilikuwa ikijiandaa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu ilipoanzishwa. Jubilei ilikuwa iadhimishwe mwaka 1955.
 Kituo hiki cha Hija kilianzishwa kwa madhumuni ya kushiriki kiroho katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 tangu tamko rasmi la Kanisa la mwaka 1854, kuwa ni nguzo ya imani kwamba Bikira Maria aliumbwa bila dhambi ya asili. Vilevile, mwaka 1958 kuliadhimishwa Jubilei ya miaka 100 tangu Bikira Maria mwenyewe alipomtokea msichana Bernadeta Subiru huko Lurdi Ufaransa mwaka 1858 na kujitambulisha kuwa yeye ndiye “aliyeumbwa bila dhambi ya asili”
#‎Bukobawadau‬
Next Post Previous Post
Bukobawadau