SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

19 June 2016

SAKATA LA RAY C KUCHUKULWA NA POLISI

Usiku wa June 16 kuamkia June 17 kuna video ya mwimbaji wa Bongofleva Ray C ilisambaa mitandaoni na kila mmoja kuzungumza habari tofauti kuhusu clip video hiyo, wapo waliosema Ray C kapata kichaa na mambo mengine mengi tu, nakusogezea mambo 4 ya kufahamu kuhusu Ray C baada ya kusambaa kwa video clip na yeye kuchuliwa na Polisi.
1- Polisi wamesema hawakumkamata Ray C bali walimpeleka hospitali kupatiwa matibabu
2- Ray C amepimwa hospitali wala hana kichaa ni mzima ana akili timamu.
3- Mkurugenzi wa uzalishaji na utafiti Clouds Media Ruge Mutahaba amethibitisha kuwa June 17 Ray amepelekwa Rehab Bagamoyo.
4- Rehab aliyopelekwa Ray C ni Bagamoyo mkoa wa Pwani, Rehab ambayo aliwahi kuishi Chid Benz wiki tano zilizopita
Tumuombee Ray C hakuna kinacho shindikana kwa Mungu.

2 comment:

Jayjoe said...

Je hayo ni MAMBO TISA (9) Kama ulivyo ahidi hapo Juu au ni Manne (4) ndugu yangu!? - Au Umechukua kwa MillardAyo pale na Kutupia tu hapa kamanda wangu... Hizi kazi zina watu wake mkuu... Hahahahaha

Anonymous said...

Usikurupuke kutuma comment kama hujui kusoma hapo juu kuna sehem mwandishi kaandika mambo tisa? Kama kiswahili imekuwa shida tena kuangalia namba tu.4 kwako ni 9.kingereza c itakuwa kilio.

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU