Bukobawadau

MAMA JUSTUCE LUGAIBULA ASHEREKEA SIKU KUU YA IDD EL FITR PAMOJA NA WATOTO YATIMA!

Katika picha Mama Justuce Lugaibula (Ma Grace) asherekea siku kuu ya Idd El fitr kwa kujumuika pamoja na watoto yatima wa kituo cha 'Nusuru Yatima' kilichopo Kashai Mjini Bukoba.
Katika tukio hili 'Ma Grace' pichani aliweza kutoa sadaka yake kwa watotoa hao pamoja na walezi wa kituo wa hicho ikiwa ni kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 
 Dada Stella Lugaibula pichani kulia akimwandalia Chakula Mama Nuru ambaye ndiye mwanzilishi wa kituo cha watoto yatima cha 'Nururu Yatima' kilichopo Kashai ndani ya Manispaa ya Bukoba
 Mama Nuru wakati akipata huduma ya Chakula
 Pichani anaonekana Mama Justuce Lugaibula akiwa tayari kupata chakula alichokiandaa kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya Idd El fitri kwa kujumuika pamoja na watato yatima wa kituo cha 'Nusuru Yatima' kilichopo Kashai-Bukoba Mjini
 Baadhi ya watoto wakinawa kwa ajili ya kuelekea kupata Chakula
Baadhi ya watoto wakiwa katika mstari  kwa ajili ya kuelekea kupata Chakula
Wakiendelea kupata huduma ya chakula kwa pamoja.
 Baadhi ya watoto wa kituo hicho wakipata msosi
Watoto hao wakiendelea kupata chakula katika kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan July 6,2016
 Siku tatu zilizopita tulishuhudia'Ma Grace' alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kutoa mwaliko wa kushiriki nao  kusherekea sikukuu hii ya leo ambapo aliweza kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama magodoro, nguo za watoto na mashuka na kuahidi kumsomesha binti mmoja wa kituoni hapo aliyechaguliwa kujiunga Kidato cha 5 na siku ya leo anajumuika nao kwa kuwaandalia Chakula na Vinywaji .
Mama Nuru pichani akiwa na mmoja wa wageni walio mtembelea wakiendelea kupata chakula kwa pamoja ikiwa ni katikakusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan July 6,2016.
 Wadau wakishiriki kupata msosi
 Dada Stella Lugaibula akifanya mawasiliano...
 Muendelezo wa matukio wakipata chakula kwa pamoja
 Mdau Abas wakati akiwakabidhi watoto hao zawadi ya Juice na Soda ikiwa ni katika  kusherehekea kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan July 6,2016
 Anaonekana mama Nuru pichani kushoto akitazama kwa macho yako kama Juice anayopewa ndilo chaguo lake....!
Bukobawadau Media tunatoa  Shukrani za pekee kwake Mama Justuce Lugaibula kwa utamaduni na upendo wa kuwasaidia watoto wanaolelewa katika vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima!
Next Post Previous Post
Bukobawadau