Bukobawadau

MAMA JUSTUCE LUGAIBULA (MA GRACE) ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA-KASHAI

 Mama Justuce Lugaibula (Ma Grace) pichani ambaye ni mkazi wa Kahororo -Kyamaizi manispaa Bukoba ametembelea kituo cha watoto yatima cha  'NUSURU YATIMA' kilichopo Kashai Mjini hapa.
Awali 'Ma Grace' alitembelea kituo hicho kwa lengo la kutoa mwaliko wa kusherekea sikukuu ya Idd na watoto yatima wa kituoni hapo,ndipo alipoguswa zaidi na hali ya mazingira na ikamladhimu kutoa msaada wa vitu mbalimbali ata kabla ya siku hiyo ,ambapo aliweza kukabidhi  magodoro, nguo za watoto na mashuka na kuahidi kumsomesha binti mmoja wa kituoni hapo aliyechaguliwa kujiunga Kidato cha 5.
 Pichani wanaonekana baadhi ya kundi la watoto hao wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa sababu nyingi,katika kundi la yatima hawa baadhi yao wamefiwa na wazazi na wapo waliozaliwa wakiwa na upungufu mwilini.
 Pichani anaonekana Mama Justuce Lugaibula (Ma Grace)wakati akikabidhi msaada huo
Mama Nuru ambaye ndiye mwanzilishi wa kituo hiki akimshukuru na kumkumbatia (Ma Grace) kwa furaha kubwa.
 Mama Justuce Lugaibula akikabidhi msaada wa mashuka
Mama Justuce Lugaibula anapata kusaini kwenye kitabu maalum cha wageni, pembeni yeke ni Bwana Abas aliyeongozana nae.
Kijana Rama akiwa amebeba baadhi ya nguo kwa ajili ya watoto hao wa kituo cha 'Nusuru Yatima' kilichopo kashai.
Kijana Rama na Bi Stera Lugaibula pichani wakishow love na watoto hao
 Mama Justuce Lugaibula  akiwa ametulia wakati anasubiria kuwaona watoto wengine wanaoishi kituoni hapo, kituo hiki kina jumla ya watoto 39 ambao baadhi yao kwa muda huo walikuwa katika shughuli mbalimbali,ikiwa panapo majaliwa watapata kusherekea sikukuu ya Idd nyumbani kwa (Mama Grace)
 So insipirational!!
 Baadhi ya watoto wa kituo hiki wakifurahi baada ya kupata msaada huo wa nguo na mashuka pamoja na magodoro
 Ndugu Abas akitoa ushirikia mara baada ya msaada huo kupokelewa.
Bukobawadu tunatoa Wito kwa watu wenye uwezo wa kifedha kujenga tabia ya kuwasaidia watu wenye uhitaji ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
God bless you Ma Grace and your family 'Omkama Abangole'!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau