Mashuhuda wamesema ajali hii imetokea asubuhi ya leo baada ya Lori aina ya Scania (Semi) yenye nambari T 360 DDU kukatika breki na kuivaa Gari aini ya Fuso yenye nambari T 920 BHW kwa nyuma na kupinduka.
Inasemekana Dereva wa Semi ilimladhimu kufanya hivyo baada ya kugundua mbele yake kuna Basi la Bunda lililokuwa likitokea stendi kuu ya Bukoba kuelekea Jijini Mwanza hivyo kufanya maamuzi aliyodhani ni salama ili kuepuka kugongana na Basi hilo.

Pichani wanaonekana mashuhuda wa ajali hiyo wakiangalia pikipiki iliyopata ajali na kupoteza uhai wa Kabeya Furgence mara baada ya kufikishwa katika hospitali ya Mkoa Kagera
Mashuhuda wakiangali pikipiki aliyokua akiendesha Kabeya Furgence aina ya Tvs Star yenye nambari T 270 EGM kabla ya kuanguka na kufunikwa na fuso tukio lililopekea kifo chake akiwa hospitalini.
Katika ajali hiyo watu wanne wamejeruhiwa na hali zao zinaendelea vizuri
Muonekano wa Contena lilikuwa limebebwa na gari aina Scania (Semi)
Wananchi wakijunufaisha kwa kuzoa Mchele uliomwagiga baada ya kutokea kwa ajali hiyo mapema ya leo jumatano July 13,2014
Muonekano wa magunia ya mchele yaliyokuwa kwenye Fuso
Mashuhuda wakiwa katika hili na lile eneo la tukio
Mwanamama pishani akiendele kujinufaisha na 'Ekimala Magazi ' mchele uliomwagisha kufuatia ajali hiyo iliyohusisha magari mawili na kupelekea kifo cha mtu mmoja aliyekuwa akienda pikipiki
Utaratibu wa kufaulisha mzigo ukiendelea
Haya ndio yaliyojiri katika tukio hili lililotokea asubuhi ya leo July 13,2014
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
Tukio lilimetokea maeneo ya Rwamishenye barabara ya Muleba usawa wa 2.5 Km kabla ya kuingia Bukoba Mjini
1 comment:
Duh hajali hii ilitisha lakini Mungu mkubwa, Mbali omkama ali tialio kabi.
Post a Comment