MPANGO WA OFISI YA WAZIRI MKUU KUHAMIA DODOMA WIKI IJAYO WAKAMILIKA
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Uratibu, na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
(Mb)amepokea Mpango Mkakati wa Kuhamia Dodoma wiki ijayo wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo Jijini
Dar es Salaam tarehe 28 Julai,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo.
Mhagama amekutana wna wakuu
wa Idara, Vitengo na Taasisi katika kukamilisha Mpango Mkakati huo ili
kukamilisha utekelezaji huo.
Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Rasilimali akiwasilisha Issa Nchasi akiwaitisha wakuu wa Idara,
Vitengo na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Mpango wa Ofisi hiyo kuhamia
Dodoma wiki ijayo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama na Naibu Waziri
anayeshughulikia ( Watu Wenye Ulemavu )Abdallah Possi pamoja na wakuu wa Idara wakifuatilia
uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa Kuhamia Dodoma wa Ofisi hiyo, leo Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Julai, 2016.
Wakuu wa Idara, Vitengo na
Taasisi wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa Kuhamia
Dodoma leo Jijini Dar es Salaam tarehe
28 Julai, 2016.
Maafisa wa Ofisi ya Waziri
Mkuu wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Mpango Mkakati wa kuhamia Dodoma katika JIjini Dar es Salaam tarehe 28 Julai,2016
katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo.
Imetolewa
na;
Afisa Habari,
Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini,
Ofisi ya Waziri Mkuu.