MWENGE WA UHURU WATARAJIA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 17.7 MKOANI KAGERA
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani shilingi bilioni 17,729,785,522 Mkoani Kagera ambapo Mwenge huo unatarajiwa kupokelewa Mkoani hapa katikaWilaya Ngara Kata ya Murusagamba mpakani mwa Mkoa wa Kigoma na Kagera tarehe 23/07/2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu atapokea Mwenge huo kutoka Mkoa wa Kigoma aidha,
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Mkoani Kagera katika Halmshauri zote za Wilaya saba na Manispaa ya Bukoba na
kupitia jumla ya miradi 68.
Katika
miradi hiyo 68 Mwenge wa Uhuru utazindua miaradi 36, utakagua au kutembelea
miradi 17, utaweka mawe ya msingi katika miradi 11, aidha, Mwenge huo utafanya
shughuli ya kugawa mizinga na kugawa hundi ili kuhamasisha shughuli za maendeleo
katika vikundi kwenye jamii.
Aidha,
mchanganuo wa gharama za miradi 68 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni kama
ifuatavyo, Serikali Kuu imechangia kiasi cha shilingi 3,811,592,405 sawa asilimia 21.5%.
Halmashauri za Wilaya zimechangia kiasi cha shilingi 854,666,220 sawa na asilimia 4.8%
Wananchi
wamechangia shilingi 5,507,747,439
sawa na asilimia 31.1% Wahisani
wamechangia shilingi 7,555,779,458
sawa na asilimia 42.6% ambapo jumla
ya gharama zote kwenye Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba katika Mkoa
wa Kagera ni shilingi 17,729,785,522
sawa na asilimia 100.
Ujumbe
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ni “Vijna ni Nguvukazi ya Taifa Washirikishwe na kuwezeshwa.”
Tujenge Jamii Maisha na Utu Wetu; Bila Dawa za Kulevya; Tanzania bila
Maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI; Inawezekana; Timiza
wajibu wako kata mnyororo wa rushwa; Wekeza katika Maisha ya baadae; Tokomeza
Malaria.
Ujumbe
huo unalenga kuwahamasisha wananchi hasa vijana kujikita katika shughuliza
uzalishaji badala ya kujihusisha na madawa ya kulevya, uteja, ngono zembe,
rushwa pia na kuchukua hatua dhidi ya malaria.
Katika
Mkoa wa Kagera Mwenge waUhuru utapokelewa Wilayani Ngara tarehe 23/07/2016 na
makabidhiano baada ya Ngara, Karagwe, Kyerwa, Misenyi, Bukoba Vijijini, Manispaa
ya Bukoba, Muleba na mwisho ni Wilaya ya Biharamulo na Mkoa utakabidhi Mwenge Mkoa
wa Geita.