Bukobawadau

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 11 JULAI, 2O16

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalim anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera kuanzia tarehe 15-16 Julai, 2016.
Katika ziara hiyo Mhe. Ummy Mwalim anatarajia kuzindua wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana siku ya Ijumaa tarehe 15 Julai, 2016. Mara baada ya uzinduzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mhe. Waziri ataelekea Wilayani Muleba kutembelea Hospitali Teule ya Wilaya ya Rubya.
Katika siku yake ya pili Mkaoni Kagera tarehe 16 Julai, 2016 Mhe. Ummy Mwalim atatembelea kituo cha kuwatunza wazee Kiilima kilichopo Wilyani Bukoba kuanzia saa 4:00 asubuhi. Kituo hicho cha Kiilima kipo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto ambapo kwasasa kinawatunza wazee 18 wanaume wakiwa 14 na wanawake 4 pamoja na watoto yatima10.
Wito kwa wananchi wote hususani wanawake wanaombwa kuhudhuria kwa wingi hasa kwenye uzinduzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kushuhudia Mhe. Waziri akizindua wodi ya wazazi ambapo mara baada ya uzinduzi wa wodi hiyo huduma kwa wazazi zitaimarika zaidi na kupunguza msongamano kwa kiasi kikubwa katika wodi ya wazazi ya zamani.
Sylvester Raphael
Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
11 Julai, 2016
Next Post Previous Post
Bukobawadau