Bukobawadau

WATEJA WAFURAHIA MICHUANO YA ICC INAYOONEKANA KUPITIA STARTIMES


 Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka akizungumza na timu ya StarTimes na maveterani wa uwanja wa Mwembe Yanga – Temeke kabla ya mchezo wa kirafiki uwanjani hapo. StarTimes iliweka kambi uwanjani hapo ikiwa ni uzinduzi wa michuano ya ICC mwaka 2016 iliyokwishaanza kutimua vumbi Julai 22 wiki iliyopita ambapo ilidhamiria kuonyesha mchuano mkali wa ‘Manchester Derby’ uliopaswa kuchezwa jijini Beijing, China lakini kwa bahati mbaya ukaahirisha kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na hivyo wateja wakapewa kutazama marudiano ya mchezo baina ya Manchester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund waliibamiza United kwa magoli 4 - 1.
 Baadhi ya wateja na mashabiki wa soka waliojitokeza kutazama mchezo wa  ‘Manchester Derby’ uliopaswa kuchezwa jijini Beijing, China lakini kwa bahati mbaya ukaahirisha kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na hivyo wateja wakapewa kutazama marudiano ya mchezo baina ya Manchester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund waliibamiza United kwa magoli 4 - 1.
 
Mmoja wa wateja waliofika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, akipata maelekezo juu ya huduma za StarTimes kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Wateja wa StarTimes na watanzania kwa ujumla wameipongeza kampuni inayouza na kusambaza visimbuzi vya matangazo ya dijitali, Starimes, kwa kuwaletea michuano ya kombe la mabingwa kimataifa au ICC mwaka 2016 moja kwa moja kupitia chaneli yake ya ST WORLD FOOTBALL.

Hayo yalisemwa na wateja mbalimbali waliohudhuria tamasha la uzinduzi wa michuano hiyo iliyoanza katika viwanja vya Temeke, Mwembe Yanga.

Katika tamasha hilo StarTimes walitinga viwanjani hapo na timu kamili ya wafanyakazi wake wa vitengo mbalimbali ambapo pia walifunga luninga uwanjani ili kuonyesha moja kwa moja mtanange wa watani wa jadi kutoka jiji la Manchester unaojulikana kama ‘Manchester Derby’ uliopangwa kufanyika jijini Beijing China lakini kutokana na hali ya hewa mbaya ikabidi uahirishwe.

Akizungumza katika viwanja hivyo Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka alibainisha kuwa, “Siku ya leo tumefika viwanjani hapa kwa lengo kubwa la kutaka kuwapa fursa wateja wetu kujionea uhondo wa michuano ya ICC inayonekana moja kwa moja kwenye visimbuzi vyetu. Michuano hii inayofanyika katika nchi ya Marekani, Ulaya, Australia na China inazishirikisha timu kubwa duniani kama vile Real Madrid, Barcelona, Manchester United na City, Juventus, Chelsea, Liverpool na nyiginezo.”

“Michuano hiyo imekwishaanza tangu Ijumaa ya wiki iliyoishia ambapo tumekwishashuhudia tayari timu kama Manchester United, Borussia Dortmund, Celtic, Leicester City, Inter Milan na PSG zimekwishatinga uwanjani. Siku ya leo tumekuja hapa kwa lengo la kuonyesha Manchester Derby lakini tunasikikita kuwa mchezo huo umeahirishwa kutokana na hali ya hewa mbaya kulikumba jiji la Beijing ambamo mchezo huo ulipangwa kuchezwa. Lakini badala yake tunaonyesha mchezo wa marudio baina ya Manchester United na Borussia Dortmund.” Aliongezea Bw. Kisaka

Meneja huyo wa Mauzo alimalizia kwa kusema, “Ningependa kuchukua fursa hii kwa kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kufurahiamichuano hii mikubwa zaidi ambayo ni ya awali au maandalizi kabla ya ligi kuu mbalimbali kuanza mwishoni mwa mwezi wa Agosti. 

StarTimes pia tunaonyesha ligi hizo ambapo wateja watafurahia mechi zote za ligi za Bundesliga na Serie A kupitia chaneli zetu za michezo za SPORT ARENA, SPORTS FOCUS, WORLD FOOTBALL, SPORT LIFE NA SPORT PREMIUM na bila kusahau ligi za Ufaransa na Ubelgiji kupita chaneli ya FOX SPORTS. 

Ili kufaidi michuano hii ya ICC mwaka 2016 wateja itawabidi kulipia malipo kiduchu ya kifurushi cha Mambo kwa shilingi 12,000/- tu na kuweza kutazama mechi zote moja kwa moja ambazo zitarajiwa kuisha Agosti 13.”

Michuano ya ICC mwaka 2016 imekwishaanza Julai 22 ambapo mechi ya kwanza iliyofungua pazia ilikuwa ni kati ya Machester United na Borrusia Dortmund ambapo Dortmund iliibamiza United kwa mabao 4 – 1. Michezo mingine iliyokwishachezwa ni pamoja na PSG kuitandika 3 -1 Inter Milan na Leicester City kuwashinda Celtic kwa mikwaju 6 – 5 ya penati baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana magoli 1 – 1 ndani ya dakika 90.


Siku ya leo Jumanne kutakuwa na mechi nyingine ambapo mabingwa wa Italia, Juventus watashuka dimbani kuwakabili timu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza katika mishale ya saa 7 mchana kwa muda wa hapa nyumbani Tanzania kupitia chaneli ya WORLD FOOTBALL ndani ya ya StarTimes pekee.

Next Post Previous Post
Bukobawadau