NAIBU WAZIRI STELLA MANYANYA AZINDUA RASMI MAFUNZO YA KKK KWA WALIMU 1770 MKOANI KAGERA
Mhandisi Stella Manyanya Akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Amantius Msole Wakiwasikiliza Walimu wa KKK
Mhandisi Stella Manyanya Mara Baada ya Kuzindua Rasmi Mafunzo ya KKK Kagera Akishuka Ngazi kuondoka.JPG
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Stalla Manyanya Akitoa Hotuba ya Uzinduzi
Walimu Waliohudhuria Mafunzo ya KKK Mkoani Kagera Wakiimba Wimbo wa Mbele ya Mhe. Mhandisi Stella Manyanya
Walimu Waliohudhuria Mafunzo ya KKK Mkoani Kagera Wakiimba Wimbo wa Mbele ya Mhe. Mhandisi Stella Manyanya
Mhandisi Stella Manyanya Mara Baada ya Kuzindua Rasmi Mafunzo ya KKK Kagera Akishuka Ngazi kuondoka.JPG
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Stalla Manyanya Akitoa Hotuba ya Uzinduzi
Walimu Waliohudhuria Mafunzo ya KKK Mkoani Kagera Wakiimba Wimbo wa Mbele ya Mhe. Mhandisi Stella Manyanya
Walimu Waliohudhuria Mafunzo ya KKK Mkoani Kagera Wakiimba Wimbo wa Mbele ya Mhe. Mhandisi Stella Manyanya
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya azindua rasmi mafunzo ya Kusoma,
Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa walimu 1770 wa Shule za Msingi 885 za
Halmashauri nane za Mkoa wa Kagera
wanaofundisha masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati kwa darasa la
tatu na la nne.
Akizindua mafunzo hayo
yanayofanyika katika Chuo cha Veta Mkoani Kagera kilichopo katika Manispaa ya
Bukoba Mhandisi Manyanya aliwapongeza walimu waliohudhuria awamu ya kwanza ya
mafunzo hayo yaliyoanza Agosti 1, 2016 kutoka katika Halmashauri za Wilaya za
Karagwe na Bukoba kwa kuitikia wito wa mafunzo hayo kwa asilimia 99%.
Pia aliwasistiza walimu hao
kuzingatia mafunzo kwa umakini kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha walimu
hao wanatoa elimu bora kwa wanafunzi ambapo mwanafunzi yeyote hawezi kupata
elimu iliyobora kama hajui kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) masomo ambayo
ndiyo msingi wa kujifunza.
Mhandisi Manyanya alisema kuwa
mafunzo ya (KKK) yanaendeshwa katika mikoa 19 ya Tanzania Bara na jumla ya
walimu 22995 watapatiwa mafunzo hayo ukiwemo Mkoa wa Kagera utakaonufaika kwa
mafunzo hayo kwa walimu 1770 ambao wanatarajiwa kuwanufaisha pia walimu wenzao
kwa mafunzo hayo ya (KKK) pindi warejeapo shuleni kwao.
Ombi, Mhandisi Manyanya aliwaomba walimu hao pia kuanzisha madarasa
ya watu wazima ili kutoa fursa kwa wananchi ambao hawakuweza kupata elimu ya
msingi ili na wao wafundishe kusoma, kuandika na kuhesabu. “Kwa takwimu za
Sensa ya mwaka 2012 ilionekana kuwa bado asilimia 29% ya wananchi kuanzia umri
wa miaka 8 hadi 50 hawajui kusoma na kuandika kwahiyo nawaombeni sana
tusaidiane kuondoa tatizo hili nchini kwetu.” Aliwaomba walimu hao Mhandisi
Manyanya.
Aidha, Mhandisi Manyanya
alibainisha kuwa nia ya Serikali ya kujenga Chuo cha VETA cha kisasa Mkoani
Kagera katika eneo la Burugo bado ipo palepale kwani imetengwa fedha katika
bajeti yake ya mwaka 2016/17 ili watoto watakaokuwa wanamaliza elimu ya Msingi
na Sekondari wakapate ujuzi wa ufundi chuoni hapo.
Katika Hatua Nyingine Bw. Benard
Merumba Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu
Bagamoyo (ADEM) alisema mafunzo ya (KKK)
yanalenga kuwafundisha walimu kutambua na kuelewa Sera mpya ya Elimu ya Mwaka 2016,
Kuitambua na kuielewa miongozo ya kufundishia masomo husika.
Vilevile walimu kukutambua mbinu
sahihi za kujifunza na kufundisha pamoja na upimaji wa ufanisi wa mada
zinazotolewa kwakutumia mbinu shirikishi. Bw.Merumba alisema pia kuwa mafunzo
hayo yanaendeshwa na wakufunzi 32 kutoka katika vyuo mbalimbali nchini.
Naye Mwalimu Fides Mnyogwa alisema
kuwa anaishukuru Serikali kwa kuliona hilo na kutoa mafunzo hayo hasa kuhusu
mitaala kwa walimu wanaofundisha masomo ya Kiswahili, kiingereza na Hisabati
kwani hapo awali walimu walikuwa wanafundisha wanavyojua kila mmoja, lakini
mara baada ya kupata mafuzo hayo sasa watapata uelewa wa pamoja na kufundisha
kwa mbinu sahihi za aina moja.
Mafunzo yanatarajia kukamilika
Septemba 15, 2016 mara baada ya Walimu kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa
wa Kagera kupata mafunzo hayo ya (KKK).