Bukobawadau

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 16 AGOSTI, 2O16 UJIO WA WAZIRI RUKUVI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera kuanzia tarehe 18-19 Agosti, 2016.
Katika ziara hiyo Mhe. William Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera siku ya Alhamisi tarehe 18 Agosti, 2016 anatarajia kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kuanzia saa 4:10 hadi saa 4:40 Asubuhi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Aidha, kuanzia saa 5:00 Asubuhi hadi saa 10:00 alasili Mhe. Lukuvi ataongea na Wananchi wote walio na kero za ardhi ambazo zimeshindikana kutatuliwa katika ngazi za Wilaya na Mkoa aidha, wawe na viambatanisho halisi na sahihi, mkutano huo utafanyika katika Manispaa ya Bukoba.
Katika siku yake ya pili Mkaoni Kagera tarehe 19 Agosti, 2016 Mhe. William Lukuvi atazindua Balaza la Ardhi la Wilaya ya Muleba kuanzia saa 03:30 hadi saa 03:50 Asubuhi mara baada ya Wajumbe wa Baraza hilo kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu katika ukumbi wa Ofisi yake.
Kuanzia saa 5:50 hadi saa 08:00 Mchana Mhe. Lukuvi atazungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba, Wenyeviti wa Baraza la Ardhi, NHC na Wataalam wa Ardhi kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba.
Wito kwa wananchi wote hususani wenye kero za muda mrefu kuhusu Ardhi na zimeshindikana kutatuliwa wanahamasishwa kuhudhuria mkutano wa Waziri ili kupata utatuzi wa kero zao. Pia vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari mnaombwa kushiriki kikamilifu katika ziara hiyo ya Mhe. Lukuvi ili kuwahabarisha wananchi hasa wa Mkoa wetu wa Kagera juu ya yale yote yatakayojili katika ziara hiyo.
Imetolewa na: Sylvester M. Raphael (Afisa Habari)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
16 Agosti, 2016
Next Post Previous Post
Bukobawadau