Bukobawadau

KAMPUNI YA ADVENT CONSTRUCTION LTD YACHANGIA MIFUKO 800 YA SARUJI KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO MKOANI KAGERA

Meneja wa Kitengo cha uzalishaji na mahusiano wa Kampuni ya  Advert Construction Ltd Kassim Masimbo (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Lucas Kinawilo ambaye ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu,alipowasili Ofisi kwake na kukabidhi mifuko 800 ya Saruji ikiwa ni sehemu ya mkono wa pole kwa wana-Kagera kutokana na maafa yaliyowakumba siku 15 zilizopita.
Bwana Kassim Masimbo wa Kampuni ya  Advert Construction Ltd akieleza namna walivyoguswa na janga hili kwa kutoa mchango mifuko 800 ya Saruji ,amesema Kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na serikali na jamii katika kutoa huduma muhimu ikiwemo kuchangia majanga mbalimbali ili kuleta maendeleo.
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Lucas Kinawilo akipokea mchango wa Saruji tani 40 iliyotolewa na Kampuni ya Ujenzi ya Advert,mara baada ya kupokea mchango huo, Mh.Kanawilo ametoa shukrani kwa Kampuni ya Ujenzi ya Advert na kuwahakikishia kuwa mchango huo utawafikia walengwa
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Lucas Kinawilo akipeana mkono na Kassim Masimbo wa Kampuni ya Advert Construction Ltd mara baada ya kukabidhi msaada huo
Kassim Masimbo wa Kampuni ya  Ujenzi ya Advert wakati akisaini kitabu maalum kabla ya kukabidhi msaada wa Saruji Mifuko 800 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi. Msaada huo uliokabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu umepokelewa leo Sep 26 na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Lucas Kinawilo
 Msaada huo umekabidhiwa mbele ya wanahabari wa vyombo mbalimbali kama inavyo onekana pichani.
Next Post Previous Post
Bukobawadau