Bukobawadau

KUTOKA KWA BABA ASKOFU KILAINI SEP 13,2016

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini kupitia ukurasa wake wa facebook ameandika;
Wapendwa,
Sisi wana Bukoba tunataka kutoa shukrani zetu za dhati kwenu nyote mliotupa pole. Inapendeza kujua kwamba kuna watu wanaojali. Katika muda mfupi tetemeko la ardhi lilileta maafa makubwa sana. Nyumba nyingi zilianguka au kuharibiwa kiasi kwamba hazikaliki. Hata mimi nyumba yangu ilipata nyufa kiasi inaweza kuanguka wakati wowote na hivyo nikashauriwa kuhama. Bahati nzuri nilipata mahala pa kuweka kichwa. Lakini kuna wengi ambao hawana pa kukimbilia. 

 Tunashukuru wote ambao wametoa misaada mbali mbali kutusaidia, Mungu awabariki na kuwazawadi.
Sis kuna makanisa kadhaa ambayo yameanguka au kuharibiwa sana kama hili la Kashozi na Ihungo umnayoyaona katika picha. Bahati nzuri Kanisa Kuu limesalimika ila vitu vidogo tu. Tumshukuru Mungu. Kuna na majengo mengine mengi yameharibika.

Tunaomba muendelee kutuombea lisije tetemeko lingine kama wanavyotabiri wataalamu. Mungu ni Mwema Kila wakati.
#TetemekoBukoba
Next Post Previous Post
Bukobawadau