Bukobawadau

TAARIFA JUU YA HATUA ZINAZOENDELEA KUCHUKULIWA NA SERIKALI KUHUSU MADHARA YA JANGA LA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

JIEPIGO kwa Ufadhili wa Watu wa Marekani Wakitoa Msaada wa Vifaa Tiba na Dawa.
Jumuiya Wazazi CCM Taifa Mara Baada ya Kutoa Msaada Wao
Kaagera Tea Company Ltd Wakitoa Mbao 250.
Kanisa la Pentecostal Wakitoa Msaada Wao kwa Mhe Kijuu
Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu Akiongoza Zoezi la Kugawa Mahitaji kwa Wahanga laeo jioni.
Mwakilishi wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) Akitoa Msaada Wao Kwa Mkuu wa Mkoa.
The Registered Trustee of Chemchem Trust Wakitoa Msaada wao wa Cementi Mifuko 600
 Wakati JIEPIGO kwa Ufadhili wa Watu wa Marekani Wakitoa Msaada wa Vifaa Tiba na Dawa.


Serikali ya Mkoa wa Kagera leo Septemba 14, 2016 tayari imepokea misaada mbalimabli ya fedha taslimu na mahitaji mbalimbali kama Sukari, Mchele, Unga, Maji ya kunywa, Sabuni, Blanketi, Shuka Maharage, matrubali, Mbao na Sementi  vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 32.

Aidha, Kamati ya Maafa ya Mkoa tayari imeanza kugawa mahitaji hayo kwa wananchi waliopatwa na janga la tetemeko na kwa sasa hawana mahala pa kuishi. Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Kashabo Manispaa ya Bukoba wamegawiwa mahita ji hayo na aliyeongo zoezi hilo ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe, Meja Jenerali Mstaafu Salim M. Kijuu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya mkoa.

Katika hatua nyingine Kamati ya Maafa ua Mkoa imeamua kutoa bati 20 na sementi mifuko 5 kwa kila mwananchi ambaye nyumba yake ilianguka kabisa au haifai kuishi tena.  Aidha, wapangaji waliokuwa wanapanga katika nyumba hizo watalipiwa kodi ya miezi na Serikali sita kila mwezi 20,000/=

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu ameandaa kikao cha harambee ya kuchangia maafa mkoani Kagera tarehe 16.09.2016 siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  kuanzia saa 3:00 Asubuhi na anawaalika wadau wote kuja kuchangia katika harambee hiyo.

Aidha kwa wale wanaotaka kuchangia lakini hawatahudhuria wanaweza kuchangia kupitia Akaunti ya Benki iliyopo CRDB inayojulikana kama “KAMATI YA MAAFA KAGERA CRDB BUKOBA” Akaunti Namba. 0152225617300. Tunawashukuru wote wanaoendelea kuchangia na Mungu awazidishie.

Imetolewa na:   Sylvester M. Raphael

                                Afisa Habari (Mkoa )

                                KAGERA

                               

Septemba 14,2016
Next Post Previous Post
Bukobawadau