Bukobawadau

WATUMISHI Watatu wa Serikali na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bukoba Wamepandishwa Kizimbani

WATUMISHI watatu wa serekali akiwemo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Bukoba mjini wamepandishwa kizimbani jana na kusomewa mashtaka mawili ya kutaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kufungua akaunti feki ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye kesi namba 239/2016.
Watumishi waliofikishwa mahakamani hapo leo ni aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Amantus Msole,mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Kelvin Makonda,Muhasibu wa Mkoa wa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja wa banki ya CRDB Tawi la Bukoba Carlo Sendwa.
Akiwasomea mashtaka yao kwenye mahakama ya hakimu mkazi ya Bukoba wakili wa serekali Hashimu Ngole alisema kuwa watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa makosa mawili kosa la kwanza ni watuhumiwa walikula njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana na jina la akaunti ya KAMATI MAAFA KAGERA yenye no.015225617300 ,ambapo wao walifungua akaunti yenye jina la KAMATI MAAFA KAGERA yenye namba no.0150225617300
Alilitaja shitaka la pili kuwa ni watuhumiwa wanashitakiwa kwa kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume cha sheria.

Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao walimwomba hakimu awapatie dhamana wateja wao kwakuwa bado ni watumishi wa serekali na wanao uwezo wa kujidhamini wenyewe na hawawezi kutoka nje ya Kagera
Hakimu Mkazi wa mahakama ya Bukoba Denis Mbelemwa alihairisha kesho hiyo hadi kesho saa tatu asubuhi baada ya kupitia upya vifungu vya sheria na kujiridhisha kama watuhumiwa wanasitahili dhamana na kutaka watuhumiwa warudishwe rumande.
"Nahairisha shauri hili hadi kesho asubuhi saa tatu nikapitie tena vifungu vya sheria,kutokana na ukubwa wa kesi hii nione kama watuhumiwa wanadhaminika"alisema
MWISHO
Next Post Previous Post
Bukobawadau