Bukobawadau

BALAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WATOA MSAADA WA MILIONI 30 KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

Na Sylvester Raphael
Balaza la Wawakilishi Tanzania Visiwani (Zanzibar) limeto msaada wa shilingi milioni 30 kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera leo tarehe 15 Oktoba, 2016.

Akikabidhi stakabadhi ya fedha hizo zilizowekwa kwenye akaunti ya Maafa ya Mkoa wa Kagera Naibu Spika wa Balaza la Wawakilishi Mhe. Mgeni Hassan Juma alisema wananchi wa Zanzibar waliguswa na janga la tetemeko lililowapata wananchi wa Mkoa wa Kagera.
Aidha Mhe. Mgeni alisema kuwa wananchi wa Zanzibar hawana cha kuwalipa wanachi wa bara kwani na wao wamewahi kuwafariji wakati walipopata maafa ya kuzama meli. “Kwa msaada huu tuliouleta tunaona ni kidogo lakini tumeona tuuwasilishe kwa ushirikiano mkubwa uliopo kati yetu.” Alimalizia Mhe. Mgeni.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu aliushukuru ujumbe huo kwa kutoa msaada wa milioni 30 na alisema msaada huo utasaidia kurejesha miundombinu mbalimbali iliyoharibiwa na tetemeko Mkoani Kagera. 
Ujumbe kutoka Baraza la wawakilishi Zanzibar uliongozwa na Naibu Spika wa Balaza hilo Mhe. Mgeni Hassan Juma aliyeambatana na Mhe. Dk. Mwinyi Haji Makame Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii na Katibu wa Kamati hiyo Bi Aziza Waziri.
Next Post Previous Post
Bukobawadau