Bukobawadau

MFALME WA MOROCCO MHE. MOHAMMED VI AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

Vikundi vya ngoma na matarumbeta vikitumbuiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya kumpokea Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI leo 23/10/2016 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi wa viongozi na wadau mbalimbali kutoka nje ya nchi wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya kumpokea Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI leo 23/10/2016 aliyewasili kwa ajili ya ziara ya siku tatu Jijini Dar es Salaam.

Ndege iliyombeba Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akielekea kumpokea mgeni wake Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI mara baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ajili ya ziara ya siku tatu ya kikazi Jijini Dar es Salaam.


Next Post Previous Post
Bukobawadau