WAKUU WA MIKOA WAENDELEA KUMUUNGA MKONO MKUU WA MKOA WA KAGERA KUWACHANGIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu
Raphael Muhunga
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu
Salum Kijuu (Aliyesimama) Akitoa taarifa ya tetemeko kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi
aliyekaa
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Raphael Muhunga (kushoto)akikabidhi Msaada kutoka Mkoa wa Katavi kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu
(Kulia)
Mkuuwa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu
Salum Kijuu Akitoa taarifa ya tetemeko
kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliyekaa
Na Sylvester Raphael
Wakuu wa Mikoa waendelea kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa mwenzao
katika kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera ambapo Mkuu wa Mkoa
wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhunga amewasilisha michango ya Wananchi
wa Mkoa huo jumla ya shilingi 13,909,600/=
Akiwasilisha mchango huo Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Mhe. Raphael Muhunga alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Katavi
waliguswa sana na athari za tetemeko lililotokea
mkoani Kagera na wametoa michango yao ili iweze kusaidia katika kurejesha
miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko hilo.
Mkoa wa Katavi unakuwa mkoa wa
pili kuwasilisha msaada kwa waathirika baada ya Mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na
Mkuu wa Mkoa wake Mhe. Zinabu Rajab Terack kuwasilisha msaada wa mahitaji
mbalimbali wenye thamani ya shilingi 41,172,000/=.
Kipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa
Katavi pamoja na wananchi wa mkoa huo ambao waliguswa na kuamua kutoa michango
yao kwa ajili ya waathirka wa tetemeko katika mkoa wa Kagera .
Aidha Mhe. Kijuu alimweleza Mkuu
wa Mkoa wa Katavi kuwa hadi sasa Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Kagera kupitia
akaunti ya maafa iliyopo CRDB Bukolba ambayo
ni 0152225617300 tayari zimekusanywa shilingi bilioni 4. Pia Mhe. Kijuu
aliwaomba wadau mbalimbali ikiwemo mikoa kuendelea kuchangia ili kuurejesha
mkoa wa Kagera katika hali yake ya awali.
Mkoa wa Kagera unaendelea kupokea
michango kutoka kwa wadau mbalimbali ili kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na
tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10/09/2016 na kusababisha vifo vya watu 17 na kujeruhi
wengine 440, aidha kusababisha nyumba 2,072 kuanguka, Nyumba 14,595 kupata
uharibifu hatarishi, na nyumba 9,471kupata
uharibifu mdogo.