Bukobawadau

WATENDAJI NA VIONGOZI WA VIJIJI WATAKIWA KUWA WAAMINIFU KATIKA SUALA LA TETEMEKO

WATENDAJI na viongozi wa vijiji wametakiwa kuwa  waaminifu katika suala la utambuzi wa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera katika kugawa misaada ya vifaa vya ujenzi ambayo vimenza kutolewa na taasisi binafsi kwa wahanga hao.
Wakizungumza na kwa nyakati tofautiofauti na mwandishi wa gazeti hili wananchi wa kijiji Mishenyi kata ya Butelankuzi wilaya ya Bukoba wathirika hao walisema kuwa misaada hiyo iliyotolewa hivi karibuni ilitolewa kwa upendeleo na wengi waliopewa hawakuwa waathirika wa janga la tetemeko na walioathirika kuachwa.
Kati ya waanchi hao Josephati Rwegoshora mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa ilitolewa mifuko mitano mitano ya simenti kwa waathirika wa kata hiyo ya Buterankuzi kwa kaya zipatazo 60 msaada uliotolewa na shirika la World Vision Tanzania lakini waliopewa sio wote waathirika.
Aliongeza kuwa kulikuwa na kujuana katika kubaini wathirika kwani viongozi wa kata walibagua baadhi ya watu na kuweka wengine ambao nyumba zao hata nyufa hazina na kusababisha waliopata madhara kuendelea kuilalamikia serikali.
 
“Hii misaada ikiwa inatolewa serikali ihakikishe inasimamia kikamilifu hili zoezi humu kuna suala la watu kujuana na undugu wakati sisi ambao nyumba zilianguka hatukuwekwa hatujui ni sababu gani imechukulia tuachwe na hawa watendaji wa kata  yetu”alisema Mwananchi huyo.
Akizungumzia malalamiko hayo Mwenyekiti wa halmashaui ya wilaya Bukoba Murshidi Ngeze alisema kuwa malalamiko hayo yapo na wamekwisha yafahamu na wamejipanga kuhakikisha kuwa misaada yote itayotolewa watahakikisha inasimamiwa kikamilifu ili kuondoa malalamiko hayo.
Aliwataka watendaji kabla ya kupokea na kugawa msaada wowote wahakikishe wanaorodhesha waathirika wote na kubandika majina yao kweye ofisi za kata au vijiji ili wananchi waende kutambua kama wametambuliwa au hawakutambuliwa.
Alingeza kuwa kama itafanyika hivyo itasaidia kutoa malalamiko ya watu yanayotolewa juu ya ugawaji wa misaada hiyo na walioathirika wote hasa walengwa watanufaika kuliko kwenda kwa wale ambao sio wahusika kama zoei hilo lilivyofanyika.
Aliongeza kuwa jumla ya kaya 60 zimepatiwa mifuko mitano katika kata Buterankuzi huku kukiwa na nyumba 99 zilizoanguka na nyumba 700 kupata athari za kubomoka katkia  kata hiyo kutokana na athari ya tetemeko iliyotokea mwezi september mwaka huu mkoani hapa.
MWISHO
Next Post Previous Post
Bukobawadau