Bukobawadau

WAZIRI UMMY ATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO MKOANI KAGERA.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kuhusu hatua iliyofikiwa na serikali katika kurejesha hali baada ya tetemeko lilitokea mkoani humo ambapo pia alimshukukuru Waziri Ummy kwa Misaada aliyoitoa wakati wanakabiliana na maafa ikiwemo, Madawa, Vifaa tiba na madktari iliyowezesha kusaidia kwa kiasi kikubwa waathirika wa tetemeko.
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kuipongeza kamati ya mkoa kwa namna walivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko pamoja na kuwahudumia waathirika
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu misaada iliyotolewa na Bohari ya Madawa (MSD) waliotoa Dawa na Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 30.
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mashuka 250 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesaili Mkoani Kagera Oktoba 7, 2016 ili kutoa pole kwa wananchi wa Kagera juu ya maafa yaliyowapata kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, 2016
Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Kagera na aliipongeza Kamati ya Maafa ya Mkoa kwa namna ilivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko pamoja na kuwahudumia waathirika.
Pia Mhe. Ummy Mwalimu alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu misaada iliyotolewa na Bohari ya Madawa (MSD) waliotoa Dawa na Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 30, Mashuka 240 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Aidha, Mhe Ummy Mwalimu alitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu kuwa Wauguzi wote nchini kupitia chama chao kijuliknacho kwa jina la TANA waliweza kuchangia waathirika wa tetemeko Kagera kiasi cha shilingi 4,203,500/= na kiasi hico kiliwekwa kwenye akaunti ya maafa ya Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mara baada ya kutoa taarifa kwa Mhe. Waziri Ummy Mwalimu kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali katika kurejesha hali baada ya tetemeko kutokea alimshukukuru Waziri Ummy kwa Misaada aliyoitoa ili kuresha hali kama ilivyokuwa awali.
Katika hatua nyingine Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alihaidi kutuma wataalamu wa mambo ya kisaikolojia kuja Mkoani Kagera ili kushirikiana na wataalamu wenzao kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wananchi
walipatwa na maafa ili waweze kurudi katika hali yao ya kawaida.

Vilevile Mhe. Ummy Mwalimu alitoa agizo kwa Mamlaka ya Maji ya Manispaa ya Bukoba kuhakikisha wanatibu maji yanayotumiwa na wananchi kwa sasa ili kusije kutokea mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu na magonjwa ya milipuko.


 
Next Post Previous Post
Bukobawadau