Bukobawadau

YALIYOJIRI LEO MAENEO YA MPAKANI ZIARA YA RAIS MSEVENI WA UGANDA OCT 4,2016

Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Leo ametoa Mabati 30,Saruji ,misumari na Saruji yenye uwezo wa kujenga nyumba ya mabati 30 kwa kila Kaya iliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi hii kwa Raia wa Uganda waliopo mpakani jirani na Tanzania maeneo ya Kashenye na Minziro na kwa kuwa eneo hilo lina nyasi aina ya (Eyonjwe) na Udongo usio na rutuba serikali yake itawafanyia mkakati wa kuwainua kiuchumi ikiwa ni hatua mbadala kutoka na Changamoto za kilimo katika Ukanda huo,Rais Yoweri mseven kaongelea madhara makubwa ya Ugonjwa wa Ukimwi katika jamii ya ukanda huo
 'Msaada huu ni nje ya zile Dola laki mbili alizotoa kusaidia tetemeko la ardhi mkoani Kagera'.
Kupitia akaunti yake yaFacebook na Twitter Rais Mseveni amesema;''Baada ya Kupata taarifa kadhaa, leo nimelazimika kufika kuwaona na kuwafariji watu wetu wa Rakai waloathirika sana na tetemeko la ardhi lilotokea September."
Kitaalam inasemekana kwamba Tetemeko la ardhi limetokea Tanzania hivyo Rakai imeathirika sana kutokana na kuwa karibu sana na Tanzania. Nimetembelea pia Vijiji vya Minziro na Lukunyu vikivyoko Kakuuto.
Tunashukuru Mungu kuwa hakuna aliyepoteza maisha kwamaana hicho tu ndo kitu chenye thamani kubwa ambayo si rahisi kurejesha.
Familia zote ambazo zimepoteza malazi zitapatiwa mabati 30, cement na misumari kama mchango wa serikali katika uwasaidia kurejea katika maisha yao ya awali.
Nimefurahishwa pia na kuboreka kwa hali ya afya ya Rakai. Sote tunakumbuka jinsi watu walivyokua wameathirika na janga la UKIMWI miaka ya nyuma. Nahimiza jitihada zaidi katika kukabiliana na janga hili.
 Wakazi wa maeneo ya kakunyu Mpakani wakimsikiliza Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda
Tujipongeze pia kwa kupatikana kwa tiba ya kansa ya kizazi, hepatitis B, na homa ya manjano pasipo kusahau tiba zenu za asili ambazo tumekua nazo siku zote.

Mwisho, tuchukulie tetemeko hili la ardhi kama funzo. Nimeshauri watu wetu wa Rakai kujenga majengo imara kutokana na jografia ya eneo lao kuwa katika ukanda wa matetetemko ya ardhi. 
Asante!
 Hiki ndicho alicho kiandindika kpitia ukurasa wake wa faceboo leo Oct 4,2016
 Credit:Bukobawadau Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau