Bukobawadau

DAWA ZA ASILI ZA WAHAYA

Mpenzi msomaji nina kukaribisha katika kujifunza mila na desturi za asili ya wahaya. Naziita mila na desturi za asili maana sasa hivi inawezekana hazipo tena, lakini mimi nazieleza kama zilivyo kuwa. Kama tulivyoona katika mada zilizo tangulia wahaya ni jamii iliyo jitosheleza karibu kwa kila kitu kulingana na mahitaji yao kwa wakati huo. Tumeona viwanda na stadi za utengenezaji wa zana mbali mbali za mahitaji ya kila siku.

Hebu leo tuone jamii ilijikitaje kwenye suala la tiba. Wahaya walikuwa maarufu sana katika suala la tiba na ukunga. Walikuwa na uwezo kutibu magonjwa yote waliyoisumbua jamii . kuanzia maumivu ya kawaida mpaka magonjwa makubwa kama kuvunjika mifupa na magonjwa ya akili. Zilifanyika mpaka operesheni ndogo za kupanua mlango wa uzazi na kugeuza mtoto aliyekaa vibaya tumboni. Kuna madaktari walioweza kuunga mifupa bila kumugusa mgomjwa.

Pamoja natiba hizo kubwa kubwa kuna tiba za kawaida ambazo karibu kila mwana jamii angeweza kuzitoa. Kuna dawa maarufu zilizojulikana kwa kila mtu na kanuni zake za kuzitoa zilifundishwa kwa watu wote. Dawa za dharura kwa magonjwa ya watoto, dawa za huduma ya kwanza kwa majeruhi na maumivu ya kawaida.

Baadhi ya dawa ambazo kila mtu alikuwa akizifahamu matumizi yake. Dawa kama Akashwagala, Omubilizi, Ekikugwa, Akakulula na Enkaka. Dawa hizi zilitumika kwa wingi katika kutibu magonjwa ya kawaida katika jamii.

AKashwagala dawa hii ilitibu magonjwa mengi, ilitibu kikohozi kwa kuchanganywa na limau. Ilitibu karibu magonjwa yote ya tumbo na kujaa kwa gesi tumboni.
 Akashwagala
 Omubilizi hii ilikuwa dawa maarufu kwa ajili ya kutuliza homa na kusokota kwa tumbo
 Ekikugwa hii ilitumika hasa kwa watoto wachanga na akina mama wajawazito kutuliza homa na kujaa kwa gesi tumboni .
 Enkaka hii ilikuwa inatibu karibu magonjwa yote ilikuwa ni dawa iliyotumika kama kinga ya magonjwa ili tumiwa hata kabla ya kuugua.
 
Kama nilivyo tangulia kueleza hizi ni baadhi ya dawa zilizo tumiwa kila siku. Na magonjwa niliyoyataja ni sehemu tu ya tiba zinazopatikana katika dawa hizi.

Katika hizi kuna dawa zimetokea kuwa maarufu hata katika kizaza hiki mfano enkaka. Kwa sasa hii dawa inajulikana kama aloe vera. Hii dawa kwa sasa inatangazwa sana, lakini kwa wahaya ilikuwa dawa ya kila siku na karibu kila shamba likuwa na mmea huu.

Mpendwa msomaji usichoke kusoma makala hizi, ili ujifunze mengi kuhusu jamii ya wahaya. Pia na kuomba usikose kutoa maoni yako kuhusu ulichokisoma hapa. Hata ulichokisoma kwenye mada nyingine ulizo wahi kusoma katika blog hii.

Tuko pamoja.

CREDIT:shafiabdunuru@mtaalamu.net
Next Post Previous Post
Bukobawadau