Bukobawadau

SHIRIKA LA NDEGE LA RWANDAIR LIMEPOKEA NDEGE YAKE NYINGINE MPYA AINA YA BOENG 737-800 LEO TAREHE 16/11/2016


Baada ya kupokea ndege mpya aina ya Airbus mwezi wa tisa mwaka huu sasa leo tarehe 16/11/2016 Shirika la ndege la Rwandair limepokea tena ndege nyingine mpya aina ya Boeing 737-800 kizazikipyayenyekubebaabiria 154.
Meneja mkazi  Tanzania ndugu Ibrahim Bukenya amesema kwa ujio wa ndege hii umetimiza idadi ya ndege kufikia kumi (10).
Ameendelea kwa kusema kuwakuanzi atarehe 8/12/2016 shirika la ndege la RwandAir litaongeza safari zakemara 14 kwa wiki badalayasasamara 11 kutokea Dar es Salaam kuelekea Kigali nakuunganisha Lagos,Accra,Abidjan,Cotonou,Libreville,Brazzaville,Douala,Kamembe,Lusaka,Johannesburg,Bujumbura,
Entebbe,Nairobi,Mombasa,Dubai na Juba.
Ndugu Ibrahim Bukenya ameendeleakwakusemakuwaShirika la ndege la RwandAir linategemea kuanzisha safari zake za kuelekea Harare,Bombayna London mwanzo mwa mwezi wa kwanza mwaka 2017.
  Ndugu Ibrahim Bukenya pichani ameendelea kwa kuwashukuru wasafiri wote washirika hilo na wadau wote kwa kushirikiana kulikuzashirika hilo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau