Bukobawadau

MBUNGE WA JIMBO LA NKENGE BALOZI DR KAMALA LEO AMEKABIDHI MADAWATI 537 KWA UONGOZI WA HALMASHAURI YA MISSENYI

 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr.Kamala leo alhamisi Dec 1,2016 amekabidhi madawati 537 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi, Limbe Mourice,Madawati hayo yametokana na fedha zilizopatikana kwa kubana matumizi ya Bunge ambapo Rais Magufuli aliagiza fedha hizo zikabidhiwe  wa Magereza na JKT ili kutengeneza madawati
 Balozi Dr.Kamala akitolea ufafanuzi amesema wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Missenyi waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya uhaba wa madawati na viti na kusababisha baadhi yao kuwa tabia ya utoro sasa watanufaika na agizo la Rais Dr.John Magufuli la kutaka wanafunzi wote nchini kuhakikisha wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati.
 Muonekano ya Madawati hayo yaliyotoka na Bunge kubana matumizi katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Safari za Nje.
 Afisa Elimu Msingi Wilayani Missenyi Bi Linda Marandu (kushoto) akikabidhi kwa Mbunge Dr. Kamala mchanganuo wa Mgao wa Madawati hao yaliotokana na Bunge la Tanzania kubana matumizi ,pichani katikati ni Joseph Rubaihuka Kaimu Afisa Elimu Sekondari
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi  Limbe Mourice wa pili kutoka kulia akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala kwa kuweza kufanikisha mradi huo na kukabidhi madawati 537 .
  Mbunge wa Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Limbe Mourice mara baada ya makabidhiano hayo yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Missenyi leo Alhamisi Dec 1,2016.
Jumla ya Madawati  417 yatatumika katika Shule za Msingi  na Madawati 120 ni kwa ajili ya SHULE Sekondari zenye uhaba wa madawati zilizomo katika kata mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya Missenyi
  Katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni  Mbunge wa Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Limbe Mourice na Mwenyekiti wa halmashauri  Projetus Tegamaisho
 Bi Linda Marandu,Afisa Elimu Msingi wakati akiongea na wanahabari.
Kushoto ni Mwanahabari Respicius John wa Radio Karagwe na kulia ni Diana Deus wa Fadeco Radio

Kushoto ni Joseph Rubaihuka Kaimu Afisa Elimu Sekondari wakati akitolea jambo ufafanuzi Mbele ya Mbunge na Wanahabari

 Mara baadhi ya Zoezi hilo kukamilika
Muonekano wa baadhi ya Madawati hayo
Balozi Dr. Balozi Dr. Diodorus Buberwa mara baada ya kutekeleza kwa asilimia 100 agizo la Rais kupitia fedha ambazo zimepatikana kutokana na kubana matumizi yasiyo ya lazima katika ofisi yake kwa lengo la kuweza kusaidia katika kuboresha sekta ya elimu,zoezi lililofanyika leo Dec 1,2016 
Pichani anaonekana Bi Karo Mwanahabari wa Mtanzania
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge akiondoka eneo la tukio mara baada ya kukabidhi kwa Viongozi wa halmashauri ya Wilaya Missenyi Jumla ya madawati 537
Mwisho ni Muonekano wa Nyumba Jengo la halmashauri ya Wilaya Missenyi leo Dec 1,2016
#Bukobawadau Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau