Bukobawadau

RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKA WAZEE KATIKA KITUO CHA KIILIMA BUKOBA

Na   Mwandishi wetu.
Bukoba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr  John Pombe Magufuli  amewatakia heri   Wazee wanaotunzwa katika  Kituo cha Kulelea Wazee  Kiilima kilichopo katika    kata Nyakato wilaya ya Bukoba  kwa kutoa vyakula mbalimbali watakavyo vitumia katka kusherehekea sikuku  ya Krismas na Mwaka Mpya 2017.

Salamu hizo zimetolewa na mkuu wa mkoa wa Kagera. Meja Jenerali mstaafu Salim Kijuu kwa niaba ya Rais , na kusema kuwa  anatambua umuhimu wa Wazee na pia yuko pamoja nao katika sherehe hizo za kumaliza mwaka 2016.
Aliwatakia heri na baraka na pia kuwataka washerehekee  Sikukuu hizo  kwa amani na upendo.

Aliwakabidhi kilo 150 za Mchele, Mafuta ya kupikia Lita 40,  Sukari na beberu la Mbuzi kwaajili ya kitoweo.
Kwa upande wake Mlezi na Mfawidhi wa Kituo cha Wazee Kiilima, Gradness Rwiza,  alisema kuwa Kituo hicho, ambacho kilianzishwa rasmi mwaka 1977 hadi sasa  kina jumla ya Wazee 25 wakiwemo Wanaume 15, Wanawake Watano na Watoto Watano.

Aidha, alimshukuru  rais Magufuli kwa msaada huo na pia kiuiomba Serikali izidi kuwakumbuka Wazee hao.
Naye Yuliana Jakobo (65) mzee anaeishi katika kituo cha kiilima alisema kuwa anampongeza John Pombe Magufuli kwa kuwakumbuka katika kipindi muhimu cha sikuku.

"Nitumie nafasi hii kwa kutuona sisi wazee kwa kutupa zawadi ya mro wa krisimasi kwani tunajiona kuwa tunathaminiwa na tunapendwa"alisema Jakobo

Jakobo alisema kuwa pia tunaishukuru serikali kwa tukumbuka kutujengea mabweni 'kwani tumekuwa tukitumia bweni moja na kulala pamoja jinsia zote sasa tumeanza kupata matumaini kwani uboleshaji wa mabweni sasa ni mzuri na umefikia hatua nzuri'.
mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau